Posts

Showing posts from July, 2021

Maestro: Ukimya wa Babra ndio uliomuondoa Manara

Image
  Mtangazaji huyo na mchambuzi wa soka kutoka Efm Maestro Ibrahim ameongeza kuwa Haji Manara alifanya kosa kuongea mambo ya Simba hadharani huenda hakujua madhara yake shida inakuja CEO @bvrbvra alitumia busara akakaa kimya bila kumjibu kitu Haji Manara ameifanyia Simba mambo makubwa sana lakini kwa hili alilofanya ilitakiwa mmoja aondoke, je kwa muliozisikia sauti ungemuadhibu nani kama wewe ungekuwa msuluhishaji Haji Manara au @bvrbvra ambaye hakuongea chochote? Kwa haya maamuzi nafikiri Simba wameonyesha ukomavu kwenye uongozi, simshauri Haji Manara arudi Simba kinachotakiwa afanye mambo yake. from Udaku Special https://ift.tt/3zYykAS via IFTTT

Diamond afurahia kufikisha viewers mil 2 kwa siku mbili, Alikiba afikisha mil 2 ndani ya siku moja

Image
  Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika kuwa Thank U Our Real Fans For 2Million Views in 2 Days …. Keep Watching #IYO Full Video. Baada ya muda mfupi Alikiba naye alifanikiwa kufikisha viewers milioni mbili ndani ya siku moja. Ikumbukwe kuwa nyimbo hizo mbili ziliingia kwenye rekodi mpya baada ya kufikisha viewers mil moja kwenye mtandao wa YouTube kwa kupishana saa moja tu. Iyo ya Diamond ambayo imeachiwa siku mbili zilizopita ilifikisha viewers milioni moja ndani ya masaa 13 huku Jealous ya Alikiba ikifikisha viewers milioni moja ndani ya msaa 12 na kuwa nyimbo za kwanza Tanzania kufikisha viewers hao ndani ya masaa machache tu. Baada ya hapo mchuano ulianza ambapo Iyo ilifikisha viewers milioni mbili ndani ya siku mbili huku Jealous ya Alikiba ikifikisha viewers milioni mbili ndani ya siku moja. Diamond katika ngoma yake ya IYO amewashirikisha wasanii kutoka nchini Afrika Kusini ambao ni Focalist,Mapara A Jazz & Ntosh Gazi huku Alikiba akimshirikis...

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari.. Ali Kiba Amburuza Diamond Platnumz Viwers YouTube Nyimbo Mpya

Image
Wimbo wa Alikia Jealous una watazamaji Milion 2.2 ndani ya siku mmoja, huku wimbo wa DiamomdPlatnum Iyo unawatazamaji Milion 2.1 ndani ya siku mbili. Msanii yupi hapo kamkimbiza mwenzie? from Udaku Special https://ift.tt/3jdXo0h via IFTTT

Ben Pol na Aliyekuwa Mchumba Wake Anarlisa Kutoja Kenya Kugawana Mali?

Image
Mtangazaji Frida Amani kutoka Clouds FM amemuuliza Mwanamuziki Ben Pol aliyekuwa mume wa Mrembo Tajiri Arnelisa kutoka Kenya kuhusu mchongo wa kugawana mali baada ya kuachana na Mrembo Anerlisa ambaye alikuwa Mke wake, majibu ya Ben Pol ni 👇🏽 “Mimi na aliyekuwa mke wangu hatukusaini chochote kuhusu mali, pili hatukuchuma chochote kwenye ndoa yetu na tatu hicho hakikuwa kipaumbele changu! Imebaki hivyo tu,” -@iambenpol • from Udaku Special https://ift.tt/3lm87bs via IFTTT

Mnyika awataka wananchi kuchukua hatua kupinga kukamatwa Mbowe

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitangaza siku ya tarehe 5 Agosti mwaka huu kama siku ya kupinga kukamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe . Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Chama hicho ,John Mnyika  amedai  kilichofanyika kwa Mwenyekiti huyo ni uendelezaji wa ukandamizaji wa demokrasia nchini. “Mbowe alikuwa kwenye kazi ya kutetea Katiba Mpya ,Mbowe alikuwa kwenye kazi ya ujenzi wa chama ,Mwenyekiti  Freeman Mbowe anapaswa kuachiwa huru mara moja” –John Mnyika “Chama kimeacha uhuru kwa wananchi , wanachama  na viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali waweze kuandaa matukio ya kupinga mashtaka ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti  Freeman Mbowe na matukio ya kudai Katiba mpya katika siku hiyo “ John Mnyika Chama hicho pia kimesema baada ya tarehe hiyo kitapanga upya ratiba za makongamano kwa ajili ya Katiba Mpya kwa nchi nzima. from Udaku Special https://ift.tt...

Ifahamu miji 5 duniani yenye gharama ya chini zaidi ya kuishi

Image
Gharama za kuishi ni muhimu unapochagua ama kutafuta mahali pa kuishi, itakusaidia kuishi raha mustarehe kwa sababu utaamua kuchagua mahali penye gharama nafuu ya vitu kama malazi, huduma za afya, gharama za usafari na vyakula. Kuna baadhi ya miji, ama nchi gharama zake za kuishi ni kubwa mno kulingana na vipato vya watu wengi. Kwa mfano majiji kama New York na San Francisco nchini Marekani gharama zake za kuishi ni za juu ukilinganisha na majiji mengi ya nchi hiyo, Afrika, Asia na baadhi ya majiji ya nchi za Ulaya. Kwa upande mwingine yapo majiji ambayo gharama zake ni za kutupwa, ni rahisi na unaweza kuishi kwa mbwembwe kwa gharama nafuu na ukapata huduma zile zile ama zinazofanana na hizo kwa ubora tofauti ila kwa gharama ya kawaida. Watu wengi hasa kutoka mataifa ya Ulaya na Marekani na wachache Asia, wanafunga safari kwenda kuishi ama kutembelea majiji ambayo gharama zake ni nafuu. Na hapa BBC inakuletea angalau majiji 5 ambayo maisha yake ni rahisi kutokana na gharama...

Mafia Hushpuppi Kwenda Jela Miaka 20

Image
Mwamba anayetajwa kuwa ni Mafia namba moja nchini Nigeria kwa kuiba pesa mitandaoni, Ramon Abbas almaarufu Ray Hushpuppi amekiri kuwa ana kosa katika makosa ya kutakatisha pesa na utapeli wa mitandaoni.   Hushpuppi; mkali wa udukuzi alikuwa tishio mitandaoni kwa kula bata na kuvaa nguo za ghali kiasi cha kubatizwa jina la Gucci Master, lakini sasa huwenda akatumikia kifungo cha miaka 20 jela. Kwa mujibu wa mwandishi maarufu nchini Marekani, Evan Ratliff wa Shirika la Habari la Bloomberg, Hushpuppi amekiri kuwa na hatia mahakamani kwa kuhusika katika utakatishaji wa pesa kutoka kwenye utapeli wa kutumia e-mail na wizi mwingine wa mitandaoni.   Jamaa huyo amekiri kutakatisha pesa katika benki mbalimbali duniani ikiwemo nchini Malta. Pia anadaiwa kutaka kutapeli moja ya timu za Ligi Kuu Uingereza kwa njia ya e-mail pamoja na kutaka kutapeli kampuni ya wanasheria ya Marekani. from Udaku Special https://ift.tt/3j9cwf3 via IFTTT

SUPER – NHESHA Ni dawa ya kutibu tatizo la sukari au jina la kitaalamu (Diabetes Mellitus)

Image
SUPER – NHESHA Ni dawa ya kutibu tatizo la sukari au jina la kitaalamu (Diabetes Mellitus) ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo Mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya Glucose katika mwili kutokana na mwili wake kukosa uwezo wa kutengeneza Insulin ya kutosha au seli za mwili wake kutumia insulin iliyopo au pengine mwili kuwa na matatizo yote kwa pamoja na kupelekea mgonjwa wa sukari kupata haja ndogo mara kwa mara (Polyuria) uhisi kiu kila wakati (Polydipsia) Na (Polyphagia). AINA YA KISUKARI Kuna aina chache tofauti za ugonjwa wa kisukari (1) ni ugonjwa wa Auto hii aina mgonjwa wa Auto hushambulia mfumo wa kinga na kuharibu seli katika kongosho ambako insulin huzalishwa asilimia 10% ya watu wenye ungonjwa wa kisukari wanayo aina hii (Auto). AINA YA PILI Hii hutokea wakati mwili wako unakuwa sugu kwa insulin na sukari hujenga katika damu yako hii husababishwa na kuwa na sukari nyingi kwenye damu yako kuliko kawaida. CHANZO CHA UGONJWA SU...

Corona yaitikisa Manchester United

Image
MANCHESTER United imelazimika kusogeza mbele mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Preston North End uliotarajiwa kuchezwa leo Jumamosi kutokana na kutikishwa na janga la Corona. Inaelezwa kuwa kuna wachezaji tisa wa Manchester United ambao wamepata Virusi vya Corona jambo ambalo limezua hofu na kuamua kuchukua tahadhari. Vipimo vilivyochukuliwa kufuatia mechi ya kirafiki ya juzi Jumatano dhidi ya Brenford ambayo ilichezwa mbele ya mashabiki 30,000, vilionyesha idadi hiyo ya waathirika katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solkjaer. Mechi hiyo ya Jumatano iliisha kwa sare ya kufungana mabao 2-2. Pia mechi ya Bretford dhidi ya West Ham inaweza isichezwe kwa kuwa Brendford nao wanafanya vipimo kutokana na kuhusika na mchezo dhidi ya United. Taarifa kutoka United jana ilieleza kuwa kuendeleza usalama dhidi ya Corona ndiyo kipaumbele chao jambo ambalo limefanya waliopata Corona wajitenge na wengine. "Kufuatia vipimo vya wachezaji wa kikosi cha kwanza tumep...

Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa Zesco wa Zambia

Image
Timu ya Yanga ipo katika hatua  za mwisho za kukamilisha  usajili wa beki wa Zesco ya  nchini Zambia, Mkongomani  Marcel Kalonda ambaye  anatumia guu la kushoto  na ni mkali katika kukaba  katika ile staili ya mtu na  mtu ‘man to man’.   Uwezo wake huo unaweza kuwa kikwazo kwa viungo wasumbufu kwenye ligi kama Clatous Chama, Luis Miquissone pamoja na mastaika kama John Bocco na Prince Dube.   Kalonda, 23, mkataba wake na Zesco unatarajiwa kumalizika Desemba 31, mwaka huu hivyo huenda akaja kuchukua nafasi ya Mghana Lamine Moro ambaye tayari Yanga imetangaza kuachana naye  Alhamisi. Yanga imepanga kukiboresha kikosi chao ili kifanye vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kocha Nasreddine Nabi ndiye anayetajwa kupendekeza jina la beki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba, kupunguza na kuanzisha mashambulizi kwenye goli la wapinzani. “Katika kikao cha Jumatano jio...

Hili Ndo Gari la Gharama Zaidi Duniani, Sawa na Nyumba 600

Image
KUMILIKI gari zuri, yawezekana ni ndoto ya kila mtu duniani, pamoja na mambo mengine kama nyumba, ardhi, kazi na vitu vingine vya thamani. Sasa aina gani ya gari, kwa ajili ya shughuli gani na la kiwango gani cha thamani inabaki kuwa jambo linalotenganisha kundi moja na lingine la wamiliki wa magari. Wasanii, wanamichezo na watu wengine maarufu dunaini mara nyingi hutumia magari ya kifahari zaidi na yenye thamani kubwa kwa sababu ya shughuli zao na namna wanavyojiweka kwenye macho ya watu wanaowafuatilia. Hata barani Afrika, inaonekana sasa kama kitu cha kawaida kwa watu maarufu wakiwemo wasanii, wafanyabiashara na wanamichezo kumiliki magari makali, ya kisasa na ya bei ya juu.   Mtandao wa Car mart Nigeria unamtaja David ‘Davido’ Adeleke kumiliki karibu magari 10 ya kifahari yakiwemo Rolls-Royce Cullinan 2019, Bentley Bentayga na Range Rover Sport. Ayodeji ‘Wizkid’ Balogun pamoja na magari mengine anamiliki Lamborghini Uru na Porsche Panamera na msanii Diamond Pla...

Je Unawahi Kufika Kilele na Kushindwa kurudia Tendo? Soma Hii

Image
Baada ya kuchambua mambo yanayosababisha upungungufu wa nguvu, kukosa ham ya tendo na maumbile madogo ya uume, leo tutachambua baadhi ya dalili na tiba. *DALILI NI KAMA:- 1.Kukosa ham ya tendo 2.Kuwahi kufika kelele ni 3.Kushindwa kurudia tendo 4.Uume kusinyaa katikati ya tendo 5.Kuchoka sana baada ya raundi moja 6.Uume kusimama kwa ulegevu *TIBA ZILIZOTHIBITISWA:- 1.GING SENG PILLS @220,000/= >Hivi ni vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza ham na nguvu za kiume hata kwa wenye kisukari 2.VIGRX OIL @220,000/= >Huongeza uume kwa 6-7 inch ndani ya wiki mbili 3.BIG PENIS, VIMAX, GOOD MAN @270,000/= (Vidonge) >Huongeza uume, nguvu za kiume na kuimarisha misuli hata kwa waliothiriwa na kujichua 4.HANDSOME UP @270,000/= >Mashine hii huongeza uume kwa saizi unayotaka pamoja na kuimarisha misuli 5.VIGA SPRAY @180,000/= >Huchelewesha kufika kileleni na kuongeza parfomance. Tiba hizi zote zimefanyiwa majaribio na zimethibitishwa. Matokeo ni uhakika na...

Serikali Yavunja Ukimiya Magari Matatu Ya Diamond

Image
MAMLAKA ya Mapato Tanzania – TRA imevunja ukimya kuhusu gharama za magari ya kifahari ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aina ya Cadillac Escalade na Rolls Royce Cullinan, IJUMAA lina stori maalum (exclusive story). Hatua hiyo imekuja baada ya Diamond au Mondi asiyeishiwa vibweka mjini, kuonekana maeneo ya Kawe na Mbezi-Beach jijini Dar, akiwa anaendesha gari lake ya kifahari aina ya Rolls Royce Callinan Black Badge 2021 bila kuwa na namba ya usajili (plate number), hali iliyozua mjadala mitandaoni kuhusu uhalali wa kutumia gari hilo bila nambari za usajili. Gari hilo ambalo iliingia nchini mwezi uliopita na kuzua tafrani mitandaoni, hasa ikizingatiwa ni mojawapo ya magari ya kifahari duniani kwani inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania. Ujio wa gari hilo pia uliwaibua viongozi wa kisiasa pamoja na wasanii wenzake ambao baadhi yao walimpongeza kwa hatua aliyofikia huku wengine wakimkejeli kuwa gari hilo ni feki, si...

Korti yatupilia mbali ombi la utetezi kesi ya Sabaya

Image
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imetupilia mbali ombi dogo la mawakii wa utetezi katika kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya la kutaka ya maelezo awali yaliyoandikwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha. Maelezo hayo ni yale yaliyoandikwa na shahidi wa sita wa Jamhuri katika kesi hiyo, Bakari Msangi (38). Mawakili hao waliomba maelezo hayo yatumike kama sehemu ya kielelezo cha ushahidi kwa kuwa utaratibu wa uwasilishwaji ulikosewa. Mbali na Sabaya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu (26) na Daniel Mbura wanaokabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha. Akitoa uamuzi huo mdogo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, alitupilia mbali ombi hilo kutokana na sababu mbalimbali baada ya la Mawakili wa Utetezi kutumika kama sehemu ya kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo. "Baada ya kusoma uamuzi wa pande zote mbili, mahakama ilirejea kwenye baadhi ya kesi katika Mahakama ya Rufani na iliainisha utar...

Jiko la mkaa laua tena Njombe ni baada ya mwingine kulala na jiko kwenye kibanda cha biashara

Image
Na Amiri Kilagalila,Njombe Edita Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa Katika kibanda chake cha biasahara. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Editha aliamua kubaki na kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwahi wateja wake wa asubuhi. Aidha kamanda Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili kuiokoa jamii. Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea  kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao. Kamanda Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda kusikojulikana. from Udaku Special https://ift.tt/3zRZ0mY via IFTTT

Rayvanny "Tupo Sawa na Hamissa Mobeto Hatuna Ugomvi"

Image
  Mwanamziki Mahili Hapa Tanzania (rayvanny ) Amefunguka kuwa WCB na Hamisa Mobeto Wapo Sawa Tofauti na Watu Wanavyo Zungumza Uko Nje. "Sisi Kama WCB Hatuna Tofauti Yoyote na (mobettohtothetop ) Tunamchukuli kama Shemeji Yetu Tuna wasiliana Nae Kama kawaidi Hatuna Ugomvi Kama Mnavyozungumza Huko Nje"-Ameongea (rayvanny ) from Udaku Special https://ift.tt/3zZn1sr via IFTTT

Mfahamu Hacker Number Moja DUNIA, Unaambiwa Kadukua Bank 217 Marekani na Kuiba Mamilioni, Amekamatwa

Image
  #UNAAMBIWA: Raia wa Algeria Hamza Bendelladj maarufu Mdukuzi mwenye tabasamu, alidukua Bank 217 Marekani na Ulaya na kutengeneza USD Milion 280 kisha alizitumia fedha hizo kutoa misaada kwa Wapalestina. Amezaliwa mwaka 1988 na alitafutwa kwa miaka mitano, akiwa kwenye Top 10 ya Wadukuzi (hackers) waliosakwa na Interpol na FBI, kirusi alichokutumia kilishambulia kompyuta zaidi ya Milioni 60 Duniani (zaidi Marekani), alidukua pia webiste ya Serikali ya Israel. Alikamatwa na yupo Gerezani Marekani baada ya Mahakama kumuhukumu April 20, 2016 kwenda Jela miaka 15, mwenzake ambaye alikuwa anashirikiana nae Raia wa Urusi Panin(27) amehukumiwa miaka 9.   from Udaku Special https://ift.tt/2X330j6 via IFTTT

Beach Plot for sale: Mbweni JKT

Image
Beach Plot for sale: Mbweni JKT Kiwanja chenye sqm 2517 kinauzwa. Kipo katika fukwe za Mbweni JKT.  Bei yake million 250, negotiable. Call 0758603077 from Udaku Special https://ift.tt/3rNQN0q via IFTTT

Msuva aweka rekodi ya kibabe Morocco

Image
  Baada ya klabu yake ya Wydad Athletic Club Jumatano hii ya Julai 28,2021 kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Morocco ‘Botola Pro League’, Simon Msuva ana kuwa mwanasoka wa tatu wa Wakitanzania kufanikiwa kutwaa ndoo nje ya nchi kwa karne ya 21. Tangu wachezaji wa kitanzania walipoanza kuchangamkia fursa ya kucheza soka la kulipwa Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Simon Msuva wote kwa pamoja wamefanikiwa kutwaa jumla ya mataji 12 ya ligi kuu na timu zao. Ulimwengu ametwaa makombe 6 ya ligi (League 1) akiwa na Tp Mazembe ya DR Congo, 1 akiwa na Al-Hilal Club ya Sudan, huku Samatta akiwa na ndoo 4 za League 1 akiwa na klabu yake ya zamani Tp Mazembe, na 1 akiwa na KRC Genk inayoshiriki First Division A huko Ubelgiji katika msimu wa 2018/2019. Huku Jalai 28 Msuva nae ameandika historia ya kuvaa medali ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Morocco ‘Botola Pro League’ baada ya timu yake ya Wydad Athletic Club kutwa ubingwa wa msimu huu wa 2020/21. from Udaku Special https://ift.tt/3jbw...

Sababu Lamine Kuvunjiwa Mkataba Yanga

Image
IMETAJWA nidhamu ndiyo sababu iliyomuondoa nahodha na beki wa kati wa Yanga, Mghana, Lamine Moro kwenye usajili wa msimu ujao. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu, uongozi wa Yanga utoe taarifa za kuachana na beki huyo mwenye umbo kubwa. Moro anaondoka Yanga akiwa amecheza michezo 21 katika Ligi Kuu Bara akifunga mabao 4 huku akipiga asisti moja pekee.Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Ijumaa, beki huyo hakuachwa na timu hiyo kutokana na kiwango, bali nidhamu ndiyo iliyomuondoa katika timu. Bosi huyo alisema kuwa Moro hivi karibuni alitofautiana na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi katika suala la nidhamu kabla ya kuondoa kambini Ruangwa, Lindi wakati Yanga inajiandaa na mchezo dhidi ya Namungo FC.Aliongeza kuwa beki huyo alitenda utovu wa nidhamu lakini akaonekana mgumu katika kuomba msamaha kwa kocha huyo. “Uongozi wa Yanga umefikia uamuzi wa kuachana na Moro baada ya kuitumikia kwa mwaka mmoja na nusu huku akiwa mkali.“ Hatua hii ya kusitisha mkataba wa beki h...

Wanaume kabla ya kuoa huangalia mwanamke mwenye sifa hizi

Image
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha. Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri. Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa. 1. Mwenye mapenzi ya kweli. Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata ...

Rais amteua mrithi wa marehemu Mhandisi Mfugale

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, amemteua Rogatus Mativila, kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akichukua nafasi ya Mhandisi Patrick Mfugale, aliyefariki dunia Juni 29, 2021. Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Julai 30, 2021, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, ambapo kabla ya uteuzi huo Mativila alikuwa ni Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mbali na huyo Rais Samia pia amemteua Prof. Yunus Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ambapo kabla ya uteuzi huo Profesa Mgaya alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR. from Udaku Special https://ift.tt/3rS1oHG via IFTTT

Ndege tumezipata kwa jasho na damu- Rais Samia

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amelitaka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kuzitunza ndege zinazonunuliwa na serikali kwa kuhakikisha linadhibiti hujuma kwa ndege hizo ili ziweze kuleta tija. Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Julai 30, 2021, wakati wa mapokezi ya ndege mpya aina ya Bombadier Dash 8 - Q400, ikiwa ni ndege ya 9 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na serikali. "Wito wangu kwenu Ndege hizi tumezipata kwa jasho na damu, nataka niwaombe watumishi wa shirika kuwa makini katika utunzaji na uhudumiaji wa ndege hizi tunazozinunua, kiufupi kudhibiti vitendo vya hujuma kwa ndege zetu zikitunzwa zitakaa kwa muda mrefu na kuleta tija iliyokusudiwa," amesema Rais Samia. from Udaku Special https://ift.tt/3zT1dhP via IFTTT

Wanafunzi wakimbia shule wakiogopa chanjo ya Corona

Image
Wanafunzi wa shule ya msingi Endiamtu iliyopo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, walipatwa na hofu ya kupatiwa chanjo ya korona na kukimbia baada ya gari la kubebea wagonjwa la kituo cha afya Mireani kufika shuleni kwao. Mirerani. Mtafaruku umezuka kwenye shule ya msingi Endiamtu Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara na wanafunzi kukimbia shuleni hapo, mara baada ya gari la kubeba wagonjwa kufika wakihofia kupata chnanjo ya corona. Wazazi na walezi zaidi ya 30 wenye watoto kwenye shule hiyo walifika mara moja shuleni hapo baada ya kusikia kuwa chanjo ya corona inatolewa kwa wanafunzi wa shule hiyo. Hata hivyo, akizungumza na wazazi hao waliofika shuleni hapo leo Ijumaa Julai 30 saa 9 alasiri, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Evetha Kyara alisema siyo habari za kweli. Mwalimu Kyara amesema madaktari wa kituo cha afya Mirerani walifika kutoa elimu ya kujikinga na corona na homa ya ini na siyo kutoa chanjo ya corona kwa wanafunzi wa shule hiyo. A...

Picha chafu zilizomfanya P Mawenge kuachika

Image
  Rapa Positive Mawenge Kiwalani Kid amefunguka msala aliowahi kukutana nao kwenye mahusiano baada ya mwanamke mmoja kumtumia picha zisizokuwa na maadili wakati huo akiwa na mpenzi wake. P Mawenge anasema kitendo hicho kilimfanya kuachwa na mpenzi wake huyo waliodumu kwenye mahusiano kwa kipindi cha miaka minne japo alijitahidi kujitetea lakini ikashindikana. "Kuna mwanamke alinitumia picha WhatsApp sasa mpenzi wangu akaona picha za ajabu ajabu zinaingia iliniletea matatizo sana,  ni mtu ambaye tulikuwa tumezoeana mpaka mnazinguana halafu ile miyayusho inakuja kudondokea kwenye wakati usio rasmi au sahihi" Aidha msanii huyo ameongeza kusema "Niliachika kwa sababu ya drama unajua ulimwengu wa sasa hivi una sababu nyingi sana za watu kugombana kwenye mahusiano na utandawazi ndio umeleta matatizo tofauti na zamani". from Udaku Special https://ift.tt/3j9HYd5 via IFTTT

Bernard Morrison Afungiwa kwa Kosa la Kushangilia, Apigwa Faini kwa kuvua Bukta Uwanjani

Image
Bernard Morrison afungiwa kwa kosa la kushangilia ,apigwa faini kwa kuvua bukta uwanjani VIDEO: from Udaku Special https://ift.tt/3yl3O3S via IFTTT

Alichosema MENEJA wa ALIKIBA baada ya JEALOUS kupata views MILIONI 1 YOUTUBE ndani ya saa 12

Image
  Alichosema MENEJA wa ALIKIBA baada ya JEALOUS kupata views MILIONI 1 YOUTUBE ndani ya saa 12 VIDEO: from Udaku Special https://ift.tt/3A8rR6P via IFTTT

BREAKING: Orodha Ya Vituo Vya Kutolea Chanjo Ya Corona Katika Mikoa Yote Nchini Tanzania na Utaratibu wa Kuomba Chanjo

Image
  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanza kufanya usambazaji wa chanjo za UVIKO-19 katika mikoa yote hapa nchini. Ugawaji wa chanjo umezingatia taarifa ya visa vya wagonjwa waliohisiwa kuwa na UVIKO-19, idadi ya walengwa kwa kundi la kipaumbele pamoja na idadi ya chanjo zilizopatikana kwa sasa. Aidha, Serikali kupitia mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA), Maabara ya Mkemia Mkuu, Maabara kuu ya Taifa na Vyombo vingine, vyote vimehakiki na kujiridhisha usalama na ubora wa hizi chanjo za Janssen kutoka Kampuni ya Johnson & Johnson nchini Marekani. ==>> BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA Kutokana na Mwongozo wa Chanjo wa Taifa dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO, ule Shirika la Afya Duniani (WHO), maelekezo ya COVAX FACILITY na upungufu wa uzalishaji wa chanjo toka viwandani, Chanjo hizi KWA SASA zinatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji mkubwa ambayo ni (1) Watumishi wa sekta ya Afya, (2)...

Kifo Habari Cha Babu wa Loliondo Chashtua, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo July 31

Image
  Kifo Habari Cha Babu wa Loliondo Chashtua, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo July 31 from Udaku Special https://ift.tt/3feJPfR via IFTTT

Aliyemuua Askari Arusha afariki akijaribu kuwatoroka Polisi

Image
Jambazi aliyemuua kwa kumkata mapanga Askari, H.2407 Constable Damasi Magoti wa kituo cha Polisi Mbughuni Wilayani Arumeru, Jacob Kideko au Ramadhani Kichwa(43) Mkazi wa Makiba amefariki dunia katika jaribio la kuwatoroka Polisi alipokuwa akisafirishwa jijini Arusha. Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, jambazi huyo alikamatwa July 27 ,2021 Mkoani Morogoro alikokuwa amejificha kukwepa Polisi na walipofika eneo la Kisongo jijini Arusha akiwa kwenye gari amefungwa pingu mkononi alijaribu kuruka kuwakimbia Polisi. Taarifa hiyo inadai kwamba mtuhumiwa alipata majeraha kichwani na michubuko kwenye mwili wake, Hata hivyo Polisi walijaribu kuokoa Maisha yake kwa kumpeleke katika hospital ya Mkoa Mount Meru ,lakini alipoteza maisha akiwa njiani. Inadaiwa kuwa jambazi huyo alikuwa akisakwa na Askari wa gereza kuu la Arusha baada ya kufungwa miaka 16 ,September 10 ,2008 lakini alitoroka mnamo April 1, 2017 akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza...

Upelelezi Kesi ya uhujumu uchumi ya Sabaya bado, ya unyang'anyi wa kutumia silaha yaendelea

Image
Arusha. Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita umeuomba upande wa Serikali katika kesi hiyo kumaliza upelelezi kwani washitakiwa wako ndani kwa muda mrefu.  Maombi hayo yametolewa leo Ijumaa Julai 30, 3021 baada ya mawakili wa Serikali kuomba kupangiwa tarehe nyingine ya kesi hiyo. Katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha, upande wa Serikali  uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula na Wakili wa Serikali Baraka Mgaya. Upande wa utetezi uliwakilishwa na Mawakili Dancan Oola na Mosses Mahuna. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27, 2021 ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Amalia Mushi. Wakili Kweka aliieleza mahakama kuwa shauri hilo lilipangwa kwaajili ya kutajwa na kuwa wanaomba tarehe nyingine kwaajili ya kutajwa shauri hilo ambapo alidai upelelezi uko katika hatua za mwisho. "Kesi leo ilipangwa ...

Wasiotaka kuchanjwa mnaweza

Image
RAIS wa Ufilipino Rodrigo Duterte, amewaonya raia wake wasiotaka kuchanjwa dhidi ya ugonjwa wa corona kusalia majumbani mwao kwa kuwa hata wakifa yeye hatajali. RAIS wa Ufilipino Rodrigo Duterte. Rais huyo amesema watu wanaokataa chanjo wamekuwa ni tisho kwa nchi kwa sababu watakuwa ni wasambazaji wanaotembea wa virusi hivyo. “Kwa wale watu ambao hamtaki kuchanjwa nawaambia msitoke nyumbani kwenu.Ukitoka nyumbani kwako ,nitawaambia polisi wakurejeshe ndani.” Utasindikizwa kurejea kwako kwa sababu wewe ni msambazaji unayetembea wa virusi hivi, Iwapo hutaki kuchanjwa basi usitoke kwako, tuwape chanjo wanaozitaka, na wasiotaka kuchanjwa basi mnaweza kufa wakati wowote, MIMI SIJALI” from Udaku Special https://ift.tt/3BWv8aQ via IFTTT