Mbowe Anavyovuna Fikra Chanya Akiwa Mahabusu..Maana ya Kitabu Anachokibeba Kila Siku Mahakamani
NOMAN Vincent Peale, alikuwa mwanathilojia na mhubiri wa Injili aliyetimiza wajibu wake ipasavyo Karne ya 20. Desemba 24, 1993, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Hakufa na kuondoka. Aliacha fikra zinazoishi. Ni fikra hizo ndizo zinamfanya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ajipambanue nazo, akitaka jumuiya ya Watanzania na duniani kote kuamini kwamba yupo imara na hatafsiri kilichopo kwa chuki. Hapa najaribu kucheza na ubongo wa Mbowe kwa lugha ya picha. Mwaka 1952, Peale alitoa kitabu kinachoitwa “The Power of Positive Thinking” – “Nguvu ya Fikra Chanya”. Shabaha iliyopo kwenye maudhui ya kitabu hicho ni kuwajenga watu kuishinda mitazamo ya hofu na kuwaelekeza kuwa na imani isiyotetereka, kwamba Mungu yupo na ndiye mwenye udhibiti wa mwisho katika kila nyakati. “The Power of Positive Thinking” kilichapwa miaka tisa kabla Mbowe hajazaliwa. Amekua na kukisoma. Bila shaka anakiamini. Anazithamini fikra za Peale. Kipindi hiki akiwa mahabusu na safari nyingi za mahaka