Vibaka nchini Ghana wamliza rapa Meek Mill
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 35 kwa sasa yuko nchini Ghana ambako alihudhuria kwaajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Muziki la Afro Nation 2022. Meek Mill alionekana kujiburudisha katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, baada ya kuenea kwa video clips mitandaoni akionekana rapa huyo nyota kutoka nchini Marekani akiendesha piki piki na vijana kadhaa wa mitaani. Hata hivyo, saa chache kabla ya onyesho lake katika tamasha la Afro Nation, alibaini na kuweka wazi kuwa vibaka wlimchomolea simu yake ya mkononi bila kujua huku akieleza kuwa anahisi ni katika kipindi ambacho walikuwa wakikatiza mitaa mbali mbali ya nchini ya Ghana. Katika chapisho kwenye kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) Meek Mill alitoa wito kwa yeyote aliyechukua simu yake airejeshe haraka. “Ni kama waliingiza mikono mfukoni mwangu nakupora simu, tafadhali nirejeshee ikiwa utaipata” ameandika Meek mill. Licha ya uchungu wa kupoteza simu yake, Inaelezwa kuwa Meek Mill hakusit...