Posts

Showing posts from January, 2023

Chelsea yavunja rekodi ya Manchester City

Image
  Klabu ya Chelsea imeweka Rekodi ya usajili nchini England, baada ya kukamilisha usajili wa Kiungo kutoka Argentina Enzo Fernandez, akitokea Benfica ya Ureno. Chelsea imeripotiwa kutumia kiasi cha Pauni Milioni 105, kama ada ya usajili wa Kiungo huyo, ambaye walimuwinda wakati wote wa Dirisha Dogo la Usajili, kwa kutuma ofa mara kadhaa. Imefahamika kuwa The Blues walikubali Dili hilo la Pauni Milioni 105 saa kadhaa kabla ya kufungwa kwa Dirisha Dogo la Usajili usiku wa kuamkia leo, baada ya ofa yao ya Pauni Milioni 100 kukataliwa. Usajili wa Hakim Ziyech wakwama Kwa Mantiki hiyo Klabu ya Chelsea inavunja Rekodi ya usajili iliyowekwa na Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, wakati wakimsajili Jack Grealish mwaka 2021, akitokea Aston Villa. Usajili huo uliigharimu Manchester City kiasi cha Pauni Milioni 100, ambacho kiliweka Rekodi ya kipekee nchini England, kabla Rekodi hiyo kuvunjwa usiku wa kuamkia leo kwa usajili wa Enzo Fernandez, mwenye umri wa miaka 22....

Jezi ya Yanga Yapondwa Vibaya- Wameiga!

Image
Siku ya jana bwana imeisha hivi..wanajagwani hao wamejikusanya zao na kuita wahandishi wa habari tayari kutambulisha jezi mpya ambazo watazitumia katika mashindano ya Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi mwaka huu. Jezi mpya hizo zimetambulishwa pamoja na mdhamini mpya kampuni ya Haier ya nchini China na deal hilo linalokaribiwa kufikia shilingi bilioni 1.5 za kitanzania. Jezi hizo zimebuniwa na Sheria Ngowi  mwanamitindo maarufu nchini Tanzania. Kama ilivyo ada watanzania bana hawajua kuvunga hata kidogo wameenda kufukunyua bana na kukuta ni copy and paste ya uzi maalumu wa Getafe CF wa mwaka 2021 kwa kusherehekea miaka 75 ya kuanzishwa kwake. Privaldinho ambae ni Menejea wa Digitali wa Yanga alianza kujigamba hivi na kuandika ” Tunatoa elimu ya ubunifu. Narudia tunatoa elimu.” Basi bwana! Si aliona kamaliza! Wabongo hao wakaanza mshushia makombora kama kawaida yao. Na hivi ndivyo walikua na haya ya kusema; Vipi wewe unazionaje? Zinafanana? Tuandikie maoni ya...

Viwanja, mradi mpya, Mapinga.

Image
Viwanja, mradi mpya, Mapinga. Viwanja vya Makazi na Biashara vipo Mapinga, km 2.5 kutoka Baobab sec. Vipo Viwanja vya mita 20/20 kwa tsh  6 milion. 20/30 kwa tsh 9 milion. 20/40 kwa tsh 12 million. 30/30 kwa tsh 14 milion. 40/50 kwa tsh 25 million. Hati miliki tunafuatilia wenyewe. Wahi sasa umiliki kiwanja aafi katka Makazi bora. Hakuna dalali/udalali. Call 0758603077 from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/mTaljWL via IFTTT

Jokate Atua Kituo cha Kazi Kipya Alichohamishiwa na Rais Samia, Amuonesha Mtoto Wake Kwa Mara ya Kwanza

Image
Jokate Atua Kituo cha Kazi Kipya Alichohamishiwa na Rais Samia, Amuonesha Mtoto Wake Kwa Mara ya Kwanza Ameweka picha yake na Mtoto na Kuandika haya: "Niediiiiiii,  Kooogwe Muendeeaa Zeze?   Niitamiwe Sana Kuiza Aha Leo.... Kangi Hata Inyi Muitamilwe Eeehh? ☺️ Asante Mheshimiwa Rais Dkt @samia_suluhu_hassan Kazi Iendelee Korogwe 🇹🇿" Jokate from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/BcZb8kf via IFTTT

Sheikh Mkuu Dar : Awachana Baraza La Maulamaa… ”Unamtetea Muhuni Kwa Kutaka Mke Ambaye Hamtaki?

Image
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amezungumzia juu ya sakata linaloendelea kuhusiana na talaka ya Dk Mwaka na mkewe huku akieleza kutoridhishwa na onyo alilopewa likidaiwa limetoka kwenye Baraza la Ulamaa. Sheikh Mkuu  ”Unamtetea Muhuni Kwa Kutaka Mke Ambaye Hamtaki? Aidha amewataka kutetea maslahi ya dini na siyo mhuni mmoja anayemtaka mwanamke ambaye hamtaki na sababu za kufanya hivyo anazieleza. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/LxP5Cpj via IFTTT

Boris Johnson: Putin Alitishia Kuniua Nilipomuonya Kuhusu Kuivamia Ukraine

Image
  Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amefichua kwamba Rais wa Urusi, Vladmir Putin alitishia kumuua endapo angeendelea na mpango wake wa kuisaidia Ukraine kabla nchi hiyo haijaivamia na kusababisha vita ambavyo mpaka sasa vinaendelea. Boris ameyasema hayo wakati akihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza, BBC ambapo ameeleza kuwa Putin alimpa vitisho hivyo, Februari 2022, muda mfupi baada ya Boris kurejea kutoka kwenye ziara yake nchini Ukraine na kuitaka Urusi iachane na mpango wa kuivamia Ukraine. “Aliniambia, Boris sitaki kukuumiza lakini kwa kombora, itachukua dakika moja tu,” amenukuliwa Boris na kueleza kuwa, alipigiwa simu na Putin na kupewa vitisho hivyo baada ya kurejea kutoka Ukraine. Alipewa vitisho hivyo, baada ya Boris kukutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky jijini Kyiv ambapo alimhakikishia kwamba Uingereza itaisaidia Ukraine endapo Urusi itaivamia. Wakati Putin akitoa vitisho hivyo, alikuwa akikanusha kwamba hana mpango wa kuivamia ...

Wanafunzi wengi shule za Dar wamepata ziro

Image
Dar es Salaam. Uchunguzi mdogo uliofanywa na Mwananchi baada kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne umebaini wanafunzi 1,308 wa shule saba jijini Dar es Salaam wamepata daraja sifuri. Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi alitangaza watahiniwa wa shule waliosajiliwa walikuwa 522,217 sawa na asilimia 97.66. Kwenye matokeo hayo, wanafunzi 63,583 sawa na asilimia 12.1 wamepata sifuri na Shule ya Sekondari Mburahati iliyofanya vibaya kwenye mtihani wa kidato cha pili kwa wanafunzi wake 229 kurudia darasa, ipo miongoni mwa zenye wanafunzi wengi waliopata daraja hilo. Sekondari ya Taifa iliyokuwa na watahiniwa 1,040 waliopata daraja sifuri ni 474, waliopata daraja la nne ni 533 na darala la pili ni wanne tu akiwamo msichana mmoja na wavulana watatu na hakuna daraja la kwanza. Katika Sekondari ya Mbagala ambayo kwenye mtihani wa kidato cha pili wanafunzi 204 wamerudia darasa, ina wanafunsi 62 waliopata daraja sufuri kidato cha nne kati ya 474 waliofanya mtihani. Seko...

Yanga Imeingia Mkataba na Kampuni ya vifaa vya umeme ya Haier Kuwa Mdhamini Mkuu

Image
Club ya Yanga SC imeingia mkataba na kampuni ya vifaa vya umeme ya Haier kuwa Mdhamini Mkuu wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika 2023. Mkataba huo utaipa Yanga Tsh Bilioni 1.5 na Haier watakaa katika jezi za Yanga kifuani badala ya SportPesa. Yanga wamelazimika kumuondoa SportPesa kwa sababu Shirikisho la Soka Afrika CAF haliruhusu timu kuwa na Mdhamini ambaye ni Mshindani wa Mdhamini wa Mashindano ya CAF (1xbet). from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/jAEhJSO via IFTTT

Yanga Muuaji , Yashusha Mvua ya Magoli Kwa Rhino Rangers

Image
Yanga imefanikiwa kuingia kibabe Hatua ya 16 Bora ya Azam Sports Federation Cup kwa kupata ushindi wa magoli 7-0 kwenye Uwanja wa Mkapa Magoli yamefungwa na Yannick Bangala, Dickson Ambundo, Kennedy Musonda (2), Stephane Aziz Ki, Farid Mussa na David Bryson Aidha, Yanga inatarajiwa kucheza na Tanzania Prisons kwenye hatua inayofuata ya michuano hiyo from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/macSh3s via IFTTT

Big Six Yaanza Kusambaratika Vipande Vipande Kabla ya Kufikia Malengo yao

Image
Kinacho endelea hivi sasa ni ugomvi wa kutupiana vijembe kati ya #wolper na #auntyezekiel ambao ni miongoni mwa waigizaji wa kike nchini wanaounda Big 6, wengine wakiwa Irene Uwoya, Wema Sepetu, Elizabeth Michael (Lulu) pamoja na Frida Kajala. Moja ya malengo ambayo walijiwekea na kuahidi kwa mashabiki wao, ni kuja na projects za pamoja, yani watarudi na filamu zao wenyewe wakiwa ndani na kufanya ishu nyingine zitazo wahusisha wao wenyewe, hii ilikuwa ni mwaka 2022. Mwanzoni ilikuwa ni ugomvi wa Wema Sepetu na Lulu ambao ulisuluhishwa na Martin Kadinda pamoja na members wengine wa Big 6. Hasa imekuwa tofauti kwa sasa ambapo Aunty Ezekiel na Wolper wameingia kwenye ugomvi mzito, ikiwemo kila mmoja kum-unfollow mwenzie, lakini pia kila mmoja kuwa na ukaribu na Ex wa mume wa mwenzie, yani Wolper kuwa upande wa Ruby na Aunty kuwa Upande wa Mwanamke aliyezaa na Rich Mitindo. Wajuzi wa mambo wanadai, Wolper yupo kwenye harakati za kupunguza waaalikwa wote ambao ni marafiki zake wa karib...

Mangungu Arejea Uenyekiti Simba Ampiga Chini Kaluwa Kwa Kura 266

Image
Murtaza Mangungu ameshinda kiti cha Uenyekiti wa klabu ya Simba kwa mara nyingine tena akimpiga chini mgombea Mwenza Moses Kaluwa kwa tofauti ya kura 266. Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia jana Januari 29 hadi lao Januari 30, 2023 Mangungu alipata kura 1311 na Kaluwa kura 1045 katika jumla ya kura halali 2356 huku kura 7 zikiharibika. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/kMNdHZb via IFTTT

Mwijaku Aguswa na Diamond Platnumz Kutotokea Kwenye Event ya Marioo

Image
Mwijaku wewe umesoma mambo ya Biashara nadhani unaelewa. Hivi sasa Diamond Platnumz sio mtu wa kutokea hovyo kwenye Events za watu, tena zilizoandaliwa na Wapinzani wake kibiashara na wenye bifu la kiukweli ukweli, tangu lini Majizzo na Diamond zikaiva? EFM na TVE wamekaa muda gani hawapigi nyimbo za Diamond then leo hii aende kutafuta nini? Kwanza Diamond angetokea hapo ange-promote Bure album ya Marioo, Mpaka sasa kuna watu hawajui kama Jana Marioo alikuwa na tukio ila Diamond angetokea kila mtu angejua kwamba Marioo ana tukio. Diamond alitokea kwa Barnaba na Jux kwa sababu waliingia Partnership. Hivi sasa Diamond hawezi kumsindikiza mtu kwenye utajiri. Ataku-support kama na yeye pia anaingiza kitu. Kama Wasafi TV na FM ndio ingekuwa Inasimamia Uzinduzi wa hiyo Album basi angetokea. @mwijaku kumbuka HARMONIZE hajatokea, kwanini yeye humlaumu? Ipo hivi, Marioo kwenda kwenye events za Diamond ni lazima na ni Muhimu, aende akajifunze mkubwa wake anafanya nini, ila Diamond kwenda kwa...

RAYVANNY amtaka MARIOO aseme ukweli kama hakutaka Kusainiwa na DIAMOND (WCB)

Image
  RAYVANNY amtaka MARIOO aseme ukweli kama hakutaka Kusainiwa na DIAMOND (WCB) VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/WMp0Fqo via IFTTT

Wanachuo Mbaroni kwa Udhalilishaji Picha za Ngono

Image
  Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Justine Masejo amesema wanawashikilia wanafunzi wawili wa Chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI), kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanafunzi wa chuo hicho kwa njia ya mtandao. ACP Masejo, ametoa taarifa hiyo hii leo Januari 29, 2023, na kuwataja waliokamtwa kuwa ni Efron Isaya (32) na Cosmas Robert (26), wote wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo hicho. Amesema, Januari 21 mwaka huu saa 11 jioni katika Chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI),  Wilaya ya Arumeru kuliripotiwa tukio la unyanyasaji wa kijinsia mwanafunzi wa chuo hicho,  (jina limehifadhiwa) kwa njia ya mtandao na wanafunzi wenzake. ACP Masejo amefafanua kuwa, baada ya kupata taarifa hiyo jeshi hilo lilianza uchunguzi wa tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata wanafunzi hao wawili. Amesema Polisi bado inaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa...

Mangungu Arejea Uenyekiti Simba Ampiga Chini Kaluwa Kwa Kura 266

Image
Murtaza Mangungu ameshinda kiti cha Uenyekiti wa klabu ya Simba kwa mara nyingine tena akimpiga chini mgombea Mwenza Moses Kaluwa kwa tofauti ya kura 266. Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia jana Januari 29 hadi lao Januari 30, 2023 Mangungu alipata kura 1311 na Kaluwa kura 1045 katika jumla ya kura halali 2356 huku kura 7 zikiharibika. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/kMNdHZb via IFTTT

Sky Tanzania Ausifia Uzinduzi Album ya Marioo "Umefana Sana Sijawahi Kuona"

Image
Uzinduzi wa #TKYK ya @marioo_tz umefana sana. Kuna namna nyimbo zake zinasound vizuri mno zikipigwa live. Huenda hii imechangiwa na bendi aliyokuwa nayo, sound nzuri (shout outs kwa @majizzo), na pia namna Dj alivyosynch na bendi. Imagine ngoma kama Mi Amor imesound vizuri kuliko original, wale back vocalists walikuwa on point kiasi cha kuhisi upo kwenye gospel concert ( I mean muziki ulikuwa mwingi na powerful sana). Amini kwamba! Ni wazi kuwa Marioo alifanya rehearsal heavy kupata ubora huu kwa namna pia yeye na dancers walivyokuwa organised jukwaani. Ukamilifu wa shughuli hii hauwezi kuongelewa bila mchango mkubwa wa wasanii waliompa support. @juma_jux alivyoimba naye na kumpa maua yake ikiwemo kumtambua Marioo kama mwandishi wa hit yake Unaniweza na walivyoperform Nice (Kiss) jukwaani. Tiktoker wa Kenya @moyadavid1 ambaye mchango katika wimbo Mi Amor unaeleweka, alipanda kwa surprise na kucheza style yake maarufu na kumpa Marioo maua. Then, kwa mbali sauti tamu ya kik...

Muigizaji Idrissultan Ametangaza Kuingiza Filamu Nyingine Katika Platform ya Netflix

Image
Muigizaji Idrissultan ametangaza kuingiza filamu nyingine katika platform ya Netflix. Hii inakuwa ni filamu ya pili kwa mkali huyo kuingia katika jukwaa hilo kubwa na maarufu ulimwenguni naye akishiriki. Filamu yake ya kwanza ilikuwa ni "Slay" ambayo iliingia kwenye jukwaa hilo mwaka 2021. Filamu hii ya pili inaitwa "Married To Work" ambayo inatarajiwa kuonekana ndani ya jukwaa hilo February 10, 2023 ambapo waigizaji wengine ni kutoka Kenya na Nigeria. Aidha, filamu ya Kitanzania ambayo pia ilishawahi kuingia katika jukwaa hilo ni "Binti" ambayo imeongozwa na Mtanzania Seko Shamte. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3PvY7hg via IFTTT

Mwimbaji nyota wa muziki nchini, msanii Ruby ameuthibitishia uma kuwa yeye ni mjamzito.

Image
  Mwimbaji nyota wa muziki nchini, msanii Ruby ameuthibitishia uma kuwa yeye ni mjamzito. @iamrubyafrica ame-share picha hiyo inayoonesha ukubwa wa tumbo lake kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii. Hitmaker huyo wa #TaiChai anategemea kupata mtoto wake wa pili baada ya binti yake wa kwanza aliyempata na mwimbaji Kusah. "Asante Mungu 🙏 #MAMAG ❤️" - ameandika Ruby kupitia kurasa zake. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/pMYrxkP via IFTTT

RAYVANNY na FEZA KESSY waongozana kama WAPENZI, sio kwa kugandana huku kama kumbi kumbi, WAMENOGA

Image
  RAYVANNY na FEZA KESSY waongozana kama WAPENZI, sio kwa kugandana huku kama kumbi kumbi, WAMENOGA VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/P5OEKZX via IFTTT

Mamlaka za Anga Kenya Waijia Juu KLM Kwa Kuzusha Uongo Machafuko ya Wenyewe Kwa Wenyewe

Image
Kenya inatarajia kuwasilisha malalamiko rasmi baada ya Shirika la Ndege la Uholanzi KLM kutangaza kufutwa kwa safari zake za Kenya na Tanzania kwa kile walichokitaja kuwa ni machafuko ya wenyewe kwa wenyewe Kenya tayari ilishawasiliana na muwakilishi wa KLM nchini humo. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Teyliqp via IFTTT

Serikali ya Tanzania Yakanusha Habari ya Kuwepo Machafuko Kati ya Tanzania na Kenya , Iliyozushwa na KLM

Image
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amekanusha taarifa zinazoenea kuhusiana na uwepo wa matukio ya kihalifu Dar es Salaam ambazo zimeripotiwa na Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM). Serikali imesema uvumi huo unaenezwa na baadhi ya taasisi za kigeni, na kwamba Tanzania haina machafuko wala matukio ya kigaidi kama inavyoripotiwa, hivyo wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku. “Tunapenda kuwahakikishia balozi zote, mashirika ya kimataifa, makampuni, taasisi, wageni na wananchi kwa ujumla kwamba eneo la Tanzania liko salama na hakuna machafuko ya wenyewe kwa wenyewe au tishio la mashambulizi ya kigaidi,” amesisitiza Msemaji Mkuu wa Serikali. Wakati huo huo, Kenya imepanga kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Uholanzi baada ya KLM kutangaza kusitisha safari zake kwa madai ya hofu ya machafuko. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/FdIoBlK via IFTTT

Randy Bangala Mdogo wa Yannick Bangala Mambo Safi Dodoma Jiji

Image
  Uongozi wa Dodoma Jiji FC umekamilisha vibali vyote vya nyota wake kutoka DR Congo Randy Bangala, ambaye hakuwahi kuitumikia klabu hiyo tangu aliposajiliwa mwanzoni mwa msimu huu. Randy ambaye ni mdogo wake Yannick Bangala wa Young Africans alisajiliwa Dodoma Jiji FC Julai 7-2022, akitokea timu ya AS Maniema Union ya DR Congo. Akizungumza suala la kiungo huyo katibu mkuu wa Dodoma Jiji FC Fortunatus Johnson amesema, kila kitu kimekamilika na wanaamini wataanza kumuona Randy akicheza. Amesema jukumu lililopo kwa sasa ni la Benchi la Ufundi kumtumia mchezaji huyo, kwa ajili ya kuisaidia timu katika Michuano ya Ligi Kuu, baada ya kutolewa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kwa kufungwa na Azam FC 4-1. “Shida ilikuwa ni kupata kibali chake cha uhamisho wa kimataifa (ITC), katika klabu aliyotokea ya Maniema Union hivyo tunashukuru kwani kila kitu kipo sawa,” “Kwa sasa kila kitu kimeenda vizuri, tunaamini Benchi la ufundi litaanza kumtumia katika michezo yetu ya Ligi Kuu, ili aisaid...

Mgogoro wa ardhi ulivyoua mifugo wangu na kuharibu mazao

Image
Katika familia yetu tumezaliwa watoto 12, wakiume tukiwa saba, huku wa kike wakiwa ni  watano. Tuliishi upendo kama ndugu maana ndivyo wazazi wetu walikuwa wanatusisitizia  kila wakati. Jina langu niNelson, mtoto wa mwisho wa mzee Nyaku, katika umri wangu wa miaka 25  nimepitia mgogoro mkubwa ambayo siweza kuja kuusahau hata pale nitakapokuwa mzee,  nao mgogoro wa ardhi baina yangu na kaka zangu. Kipindi baba yetu, Mzee Nyaku anafariki, aliachia Wosia kuwa mimi ndio nitarithi eneo  la shamba ambalo ipo nyumba yetu, pia nyumba itakuwa yangu kwa sababu mimi ni  mtoto wa mwisho.  Jambo hilo halikuwapenda kaka zangu, walisema Kwa vile mimi  nilikuwa karibu sana na Baba ndio nilitumia fursa hiyo kuandika Wosia huo na sio Baba. Ni jambo lilinishangaza kwa maana sikuwahi kujua kama kuna siku Baba aliandika  Wosia, na sijawahi kumshawishi kivyovyote kunipa mali hizo. Bali nachojua mtoto wa  mwisho ndio hupewa hivyo, ukizingat...

Waarabu Watuma Mashushushu Yanga Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika

Image
KOCHA Mkuu wa Klabu ya US Monastir ya Tunisia, Darkov Novic ameweka wazi kuwa wanatambua wapinzani wao Yanga ni miongoni mwa timu bora katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini mipango yao ni kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa kwa kuwa wanawajua vizuri na wamekuwa wakiwafuatilia wanapocheza. Novic ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga inayonolewa na Kocha Nasreddine Nabi raia wa Tunisia katika  unaotarajia kupigwa Februari 12, mwaka huu nchini Tunisia. Yanga ambao inaenda kwenye mchezo huo ikiwa inaongoza ligi kwa pointi 56 wakati wapinzani wao hao wakiwa katika michuano hiyo wakiwa katika nafasi ya kwanza katika kundi B wakiwa na pointi 22 kwenye ligi kuu ya nchini humo. Yanga kwa asilimia kubwa ilikuwa ikitegemea mabao ya Fiston Mayele na sasa wamemuongeza straika mwingine Kennedy Musonda aliyejiunga nao kwenye dirisha dogo lililofungwa Januari 15, mwaka huu. Hivyo Novic na wa...

Man City yaitupa nje Arsenal FA Cup

Image
Manchester City imewatupa Arsenal nje ya michuano ya Kombe la FA ambao ni washindani wao katika Ligi Kuu ya England (EPL). Goli pekee la dakika ya 64 la beki Nathan Ake lilitosha kuipa City ushindi ikikutana na Arsenal kwa mara ya kwanza katika msimu huu ambapo kwenye EPL bado hazijakutana. Ushindi huo unaiweka City katika nafasi nzuri ya Kisaikolojia pindi itakapokutana tena na vinara hao wa EPL katikati ya Februari mwaka huu kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa ligi. Guardiola ameendeleeza ubabe dhidi ya Arteta ambaye alikuwa msaidizi wake, katika kile kinachoonekana kuwa mwanafunzi hawezi kushinda mwalimu. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/oYf2DbU via IFTTT

Mwili wa Nemes Tarimo Aliyefariki Vitani Ukraine Waagwa Bila Kufungua Jeneza

Image
Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo ambaye alifariki October 24,2022 akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group tayari umeagwa nyumbani kwa Familia Mbezi Dar es salaam baada ya kupokewa katika Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere Dar es salaam leo January 27,2023 ambapo unatarajia kusafirishwa leo hadi Mbeya kwa maziko. Familia imesema kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao jeneza halitofunguliwa hivyo Ndugu, Jamaa na Marafiki wameaga picha na jeneza ““Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu tutatumia mtindo wa kuaga sanduku pamoja na picha hatutaweza kulifungua sanduku kwasababu zilizo nje ya uwezo wetu” Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Tanzania iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki mapema Wiki hii, Nemes alifariki akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group akiwa anatumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka saba alichofungwa kwa makosa ya kihalifu. Waz...

Mechi Kali, Odds Kubwa Meridianbet

Image
Wikiendi hii ni ya kibabe Zaidi ikisindikizwa na Odds bomba na kubwa kutoka Meridianbet, ni FA Cup, Serie A, La Liga, Ligue 1 na Bundesliga zote kutimua vumbi kwenye viwanja tofauti Jumamosi na Jumapili. LALIGA ya moto sana, Barcelona kinara kwenye msimamo atakuwa ugenini dhidi ya Girona, ikumbukwe mchezo uliopita wa Barca alipata ushindi mwembamba. Wakati huo Sevilla akiwa na hali mbaya kwenye msimamo wa ligi nafasi ya 15 na alama 18, atamkaribisha Elche kibonge wa Ligi mwenye pointi 6 tu. Wapinzani wakubwa wa Barca, Real Madrid wanahitaji ushindi dhidi ya Real Sociedad waongoze ligi kwa tofauti ya magoli endapo vijana wa Xavi watapoteza mchezo wao. Odds za Meridianbet Madrid ana 1.68 kwa 4.80 ya Sociedad. Jurgen Klopp mwenye msimu mgumu atakutana na Brighton kwenye mchezo wa FA Cup huku mechi ya kwanza alipoteza kwa bao 3-0. Liverpool ana odds ya 2.45 dhidi ya 2.55 ya Brighton. Suka mkeka wako na Meridianbet. Wababe wa Bundesliga Bayern Munich watashuka kwenye dimba lao la A...

Wafugaji 27 wafariki kwa kulipukiwa na bomu machungani

Image
Takriban Wafugaji 27 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika eneo lenye mivutano ya kikabila na kidini nchini Nigeria. Kwa mujibu wa Kamishna wa polisi wa Nasarawa, Maiyaki Muhammed Baba amesema Wafugaji hao, ambao walikuwa wakichunga mifugo, walikuwa katika kijiji cha Rukubi kilichopo kwenye mpaka kati ya majimbo ya Nasarawa na Benue. Moja kati ya matukio ya mauaji ambayo yaliwahi kutokea nchini Nigeria. Picha ya The Telegraph. Amesema, “Tumegundua watu 27 waliuawa katika mlipuko wa bomu pamoja na ng’ombe kadhaa, alisema na watu wengi walijeruhiwa na idadi ya vifo inaweza kuongezeka na tayari wataalam wa mabomu wameanza kuchunguza chanzo cha mlipuko huo.” Chama kinachowakilisha wafugaji, kimesema mlipuko huo ulisababishwa na shambulizi la anga la kijeshi, huku kukiwa hakuna taarifa za kundo lolote la uasi lililodai kuhusika na shambulio hilo lililoacha simanzi na vilio kwa jamaa za marehemu. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1Y5lJg...

Una Mvi Kichwani au Kwenye Ndevu na Unataka Kuziondoa Milele? Tumia Dawa Hii

Image
Vipo vyanzo vingi vya mvi lkn baadhi ni KUCHOKA KWA HOMONI, DAWA KALI, UMRI, KURITHI N.K Wengi wanasumbuliwa na mvi na sasa tumeleta suruhisho. Dawa hii ni ya kupaka kwenye ngozi ya sehem zote zenye mvi na zinaondoka moja kwa moja. BIGEN inasambazwa na NATURAL BEAUTY CO L.T.D kote duniani @240,000/= tu KUMBUKA matokeo ni uhakika na GARANTII PIA TUNATIBU:- *Kukosa hamu ya TENDO *Uume mdogo *Kushindwa kurudia TENDO *Kushindwa kutungisha mimba *Uume kusimama legelege >WENICK CAPSULES (270,000/=) Vidonge vya kuongeza uume, nguvu, na kuimarisha misuri >GIN SENG (240,000/=) Hii huongeza ham ya tendo, nguvu na uwezo wa kurudia tendo la ndoa >MAX MAN GEL (240,000/=) Hii huongeza urefu na upana wa uume (wiki 2) >VIGA SPRAY (180,000/=) Hii huchelewesha kumaliza tendo WEKA ODA KWA:- Call/Whatsapp no (+255) 0759029968 0659618585 TAHADHARI:- Hakikisha unapatiwa risiti yenye mhuri na GARANTII ili kuepuka bidhaa feki mitandaoni Follow us, IG, Y/TUBE A...

MAJANI awajibu BABALEVO, SALLAM, afunguka KAJALA alivyomfanya achukie muziki, ukaribu tena na PAULA

Image
MAJANI awajibu BABALEVO, SALLAM, afunguka KAJALA alivyomfanya achukie muziki, ukaribu tena na PAULA VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/TjWYtvl via IFTTT

Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo Aliyefariki Vitani Ukraine Umewasili Tanzania

Image
Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo ambaye alifariki October 24,2022 akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group umewasili katika Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere Dar es salaam asubuhi ya leo Ijumaa January 27,2023 ambapo utaagwa na kusafirishwa hadi Mbeya upande wa Mama yake kwa ajili ya maziko. Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Tanzania iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax mapema Wiki hii, Nemes alifariki akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group akiwa anatumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka saba alichofungwa kwa makosa ya kihalifu. Waziri Tax alinukuliwa akisema “Tarimo akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha lakini kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita na umauti ulimkuta October 24,2022 na Wizara ikawasiliana na Serikali ya Urusi ili kukabidhiwa mwili” “Neme...

Takribani Watu 142 Wajizolea Ajira Meridianbet

Image
  ZAIDI ya watanzania 142 wamenufaika na ajira kupitia Meridianbet Tanzania, ikiwa ni moja ya ndoto ya kampuni hiyo inayotoa huduma za michezo ya kubashiri mtandaoni. Akizungumza katika uzinduzi wa duka la Meridianbet lililopo Mtaa wa Tandika Majaribio, Temeke, Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Meridianbet Tanzania, Matina Nkurlu, alisema kuwa kama kampuni, wana malengo madhubuti ya kimkakati ya kutengeneza ajira za moja kwa moja kwa watanzania wengi wenye uhitaji mkubwa kwa sasa na kwa baadaye. “Hatimaye leo tumezindua duka la Meridianbet hapa Mtaa wa Tandika Majaribio, Wilaya ya Temeke, baada ya uzinduzi wa duka hili, tunatumaini litatoa ajira zaidi kwa ndugu zetu ambao watafanya kazi hapa na maduka yetu mengine zaidi ya 18 yaliyopo maeneo tofauti hapa Tanzania. “Mpaka sasa Kampuni ya Meridianbet inayotoa huduma za michezo ya kubashiri mtandaoni, imesaidia kutoa ajira kwa zaidi ya watanzania 142 ambao wanafanya kazi kwenye maduka yetu yaliyosam...

Meli ya Tanzania Yapinduka katika Bandari ya Assaluyeh Kusini mwa Iran

Image
Meli ya mizigo ya Tanzania iitwayo Anil imepinduka katika bandari ya Assaluyeh Kusini mwa Iran Siku ya Jumanne, Januari 24 kutokana na mpangilio mbaya wa Makontena kwenye bodi. Ajali hiyo imetokea katika Bandari inayohusika na kemikali za petroli na gesi zinazozalishwa nchini Iran iliyopo kilomita 950 kusini mwa Tehran. Katika taarifa iliyotolewa na IRNA, tovuti rasmi ya habari ya Iran, ilifichuka kuwa wafanyakazi wa Meli waliokolewa na kupelekwa kwenye eneo salama na timu ya uokoaji. Maelezo zaidi bado hayajatolewa. Biashara ya Shehena ya kila mwaka kati ya Tanzania na Iran ni chini ya dola milioni 100 lakini mauzo ya nje na uangizaji umepungua tangu tangu Marekani ilipoweka vikwazo kwenye mafuta na benki ya Iran. Meli hiyo ilikuwa na wafanyakazi 12 na wametoka salama. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/0XSZdbg via IFTTT

Una Mvi Kichwani au Kwenye Ndevu na Unataka Kuziondoa Milele? Tumia Dawa Hii

Mateso, vifungo, kufilisiwa vimejenga upendo Chadema’

Image
Siku chache zilizopita Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetimiza miaka 30 tangu kilipopatiwa usajili wa kudumu Januari 21, 1993. Chadema kimekuwa kikiimarika kila kukicha, licha ya kupitia katika wakati mgumu katika uendeshaji wake, licha ya changamoto hizo bado kimekuwa mioyoni mwa wananchi na kimbilio la wengi. Ni furaha kubwa kwa chama chetu, Chadema kufikisha miaka 30 kutoka kiliposajiliwa. Ninawashukuru sana wale wote wenye maono ya umuhimu wa kupigania mfumo wa vyama vingi na demokrasia. Miaka 30 iliyopita mimi nilikuwa bado mdogo sana. Lakini ninaweza kuwaza hali ilikuwaje nikilinganisha na sasa.Ndio sababu napata wajibu wa kufurahi na kuamini kuwa kuna watu wengi, hasa waasisi ambao majina yao pengine hatuwezi kuwataja na kuwakumbuka, lakini ustahimilivu wao na kuamini kesho bora umejenga chama imara sana nchini. Nilikuwa mpenzi wa siasa tangu nikiwa mtoto na wakati wa harakati za Hayati Mzee Lyatonga Mrema nilijikuta nimekuwa mfuasi wa siasa zake, ni...

Nimeweza kumthibiti mume wangu asichepuke

Image
Jina langu ni Asia, nimeolewa ni na watoto wanne na mume wangu wa ndoa, Jamal,  tulifunga miaka tisa iliyopita, kwa miaka mingi tuliishi kwa upendo na amani ndani ya  nyumba bila kadhia yoyote.  Majirani walivutiwa sana na jinsi ambavyo tulikuwa tukiishi pamoja, nguzo pekee  iliyotuongoza maisha ni uaminifu ndani ya ndoa, hakuna ubishi kwamba uaminifu  ukikosekana kati ya wawili basi mambo huanza kuharibika.  Licha ya mapenzi moto moto niliyokuwa nampa mume wangu na ambayo yeye alikuwa  akinionyesha, bado ndoa yetu kuna kipindi ilipitia kipindi kigumu hadi nikafikiria siku  moja niondoke nirudi kwa wazazi wangu.  Hiyo ilikuwa ni baada ya mimi kujifungua mtoto wetu wa pili, mume wangu ghafla  alibadilika na akaanza kurejea nyumbani akiwa amechelewa sana tofauti na ilivyokuwa  hapo awali.  Kila nilipojaribu kumuuliza alipokuwa hakuwa na majibu yenye kueleweka  zaidi ya kusema yeye ni Baba mwenye nyumba, hi...

Ishu ya Kocha wa Simba Roberto Oliveira, Maswali Ni Mengi Kuliko Majibu

Image
“KOCHA Mkuu, Roberto Oliveira ameondoka usiku huu kwenda kwao Brazil kwa shughuli binafsi za kifamilia na anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.” Hii ni taarifa fupi ambayo ilitolewa na uongozi wa Simba kupitia vyanzo vyao rasmi vya taarifa usiku wa kuamkia jana Jumanne. Taarifa hii ilipokelewa kwa mitazamo tofauti na wadau wengi wa soka hususan mashabiki wa Simba, wapo ambao walionekana kumtakia kila la heri kocha huyo na kumuombea safari njema ikiwemo kurudi salama. Lakini pia wapo ambao bila kujali ni shughuli gani imempeleka kwao kocha huyo waliona kama hiyo ni ahueni kwa timu yao. Licha ya kwamba haijawekwa wazi ni shughuli gani zilizompeleka Robertinho Brazil, lakini tayari mitandaoni kumeanza uvumi usio rasmi kuwa tayari ni makubaliano ya pande mbili na huenda kocha huyo asirudi tena. Waswahili waliwahi kusema kuwa lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja, hivyo binafsi sipendi kupotezea tu taarifa hizi hewani. Tuna nafasi ya kusubiri na kuona ikiwa n...

Rais Samia Afanya Uteuzi Wa Wakuu Wa Wilaya 37 Wapya, Wengine Awahamisha

Image
Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya Wapya 37, kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 48 na wengine 55 kubakia kwenye vituo vyao vya kazi. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa kati ya wakuu wa wilaya hao 140, wanawake ni 40 na wanaume ni 100.               from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/TmBZHvE via IFTTT