Mkataba wa Messi wavuja, Barca wageuka mbogo
Barcelona imesema kuwa itachukua “hatua za kisheria” dhidi ya gazeti la Uhispania la El Mundo baada ya kuchapisha maelezo kuhusu mkataba wa mshambuliaji, Lionel Messi wa pauni milioni 492. Barcelona vs Bayern Munich: End Of An Era As Barca Humiliation Makes Revolution The Only Option | Football News Barcelona ilikanusha kuhusika kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hizo. Kwa mujibu wa El Mundo, mkataba wa Messi wa miaka minne ulikuwa wa thamani ya takriban euro 555,237,619 hadi Juni 30, 2021. Hii inamaanisha kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 33, atakuwa anapokea pauni milioni 123 kwa msimu. Barcelona imesema katika taarifa iliyotoa kuwa “inasikitishwa na uchapishaji wa maelezo hayo”. Na kuongeza kuwa: “FC Barcelona haihusiki kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hiyo na itachukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya gazeti la El Mundo, kwa uharibifu wowote ule ambao huenda umetokea kwasababu ya taarifa hiyo. “FC Barcelona imeonesha kumuung...