Mondi Kibo, Konde Boy Mawenzi
Yes Mondi yupo juu zaidi, lakini chini yake kuna Konde Boy. Baada ya hapo kuna gepu kubwa sana mpaka kuwakuta wengine. Bahati mbaya zaidi hata wasanii wameamua kuwa mashabiki. Yaani kuna Team Mondi na Team Konde ya wasanii wenzao. ADVERTISEMENT Jamaa wapo juu pale. Yes Mondi yupo juu zaidi, lakini chini yake kuna Konde Boy. Baada ya hapo kuna gepu kubwa sana mpaka kuwakuta wengine. Bahati mbaya zaidi hata wasanii wameamua kuwa mashabiki. Yaani kuna Team Mondi na Team Konde ya wasanii wenzao. Mlima Kilimanjaro una vilele viwili, Mawenzi na Kibo. Yes! Ni mfano kwa wasanii hawa waliopo vileleni wakiwatazama wenzao kwa chini mitaa ya Marangu. Ukifuatilia mitikasi zao tu kupitia mitandaoni kama Insta. Utaona masela hawa namna wanavyoonyesha kwa vitendo matumizi ya noti wanazoingiza. Noti, faranga, mkwanja, mapene, mawe, shilingi, paundi, dola unaweza kuita utakavyo. Ndiyo kipimo rahisi zaidi cha mafanikio kwa wasanii na sanaa. Heshima ni moja, utajiri ni jambo lingine tofauti kabi...