Na Josefly “Alikuwa mtoto mwenye sura ya mvuto, mpole na mwenye nidhamu. Ilikuwa nadra kutazamana naye moja kwa moja machoni. Alikuwa na aibu, msikivu na neno lake halikutoka kinywani mwake bila mpangilio,” alisema Bi. Alia Ghanem, mama mzazi wa Osama Bin Laden, aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda akielezea maisha ya utotoni ya mwanaye, miaka nane baada ya kuuawa na makomando wa Marekani waliomsaka kila kona ya dunia kwa kipindi cha miaka kumi. Kwa mujibu wa mama huyo ambaye amebarikiwa kuishi hadi leo, tangu alipomzaa mwanaye Osama, Machi 10, 1957 katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia, aliiona baraka na neema kwenye maisha ya mwanaye. Kila alipokuwa akivuka rika moja, alionesha kuwa na upeo wa hali ya juu. Darasani alikuwa na akili za kipekee na alifanikiwa kumaliza Shahada ya Uchumi kwa ufaulu mzuri katika Chuo Kikuu Cha King Abdulaziz kilichoko Jiddah, Saudi Arabia. Akiwa na umri wa miaka 20, alianza kuonesha makucha ya uwezo wake na alifanikiwa kuwa na ush...