
MTU mmoja ameuawa na Jogoo wake aliyekuwa amefungwa kisu mguuni kwa ajili ya mchezo uliopigwa marufuku wa kupambanisha jogoo Kusini mwa India. Mmiliki wa jogoo alichomwa kisu usawa wa kati ya tumbo na nyonga wakati kuku huyo akijaribu kutoroka. Mwanaume huyo alipoteza maisha akiwa njiani kuelekea hospitali kwasababu ya kupoteza damu nyingi. Polisi hivi sasa wanawatafuta watu wengine 15 waliohusika kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyika kwenye kijiji cha Lothunur jimbo la Telangana wiki hii, Kuku huyo alishikiliwa katika kituo cha polisi kabla ya kupelekwa shambani. Polisi wamesema mnyama huyo alikuwa akitayarishwa kwa ajili ya kushiriki mpambano alipojaribu kutoroka. Mmiliki alijaribu kumkamata lakini alichomwa na kisu hicho chenye urefu wa sentimita 7 kilichokuwa kimefungwa kwenye mguu wa kuku huyo wakati wa purukushani hizo. Wale waliohusika katika tukio hilo wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kutokusudia,...