Posts

Showing posts from April, 2022

Morrison Ashikiliwa na Polisi Kwa Madai ya Kujeruhi Shabiki

Image
Mchezaji wa Simba, Bernard Morrison anashikiliwa katika kituo Cha Polisi Cha Chang’ombe jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumjeruhi shabiki wa Yanga na kitu chenye ncha kali. Wasafi Media imezungumza na Mkuu wa Kituo Cha Polisi Chang’ombe, ASP Mohammed Simba ambapo amethibitisha kupokea kesi hiyo “Ndio tumepokea hiyo kesi na tunaendelea na mahojiano tukikamilisha tutawajulisha,” Tukio hilo limetoka mara baada ya Derby ya Kariakoo kutamatika katika uwanja wa Benjamin Mkapa hii leo. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/JY5KIn8 via IFTTT

Morisson azomewa kwa Mkapa

Image
  MSHAMBULIAJI wa Simba, Bernard Morisson amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na mashabiki wa Yanga katika mchezo wao dhidi ya Yanga ukiendelea kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa. Kuzomewa kwa Morrison ni baada ya kocha wa Simba, Pablo Franco kumtoa dakika 54 na nafasi yake akiingia Kibu Denis wakati huo huo Sadio Kanoute alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mzamiru Yassin. Muamuzi msaidizi wa nne Elly Sasii aliponyanyua kibao cha kubadilisha wachezaji ilipoonekana namba ya Morrison mashabiki wa Yanga walianza kumzomea. Mchezaji huyo hakuonyesha kujali kwani alitoka bila kuwa na presha yoyote huku akiwa ameinamisha kichwa chini.   Morrison katika mchezo huo alikuwa na wakati mgumu chini ya Kibwana Shomari na hata alipohama upande kwenda kulia alikutana na mabeki Djuma Shaban na Dickson Job. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/T9Sb6yE via IFTTT

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH OSTADH RAMADHANI NASORO anapatikana mkoani MOROGORO

Image
Ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu Anatibu kwa kutumia visomo na dua na dawa za miti shamba pia  UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika. ............................... JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio? Wasilina na  OSTADH RAMADHANI NASORO ujionee muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 72 TU.  ............................... Umekimbiwa na Mumeo, mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.  Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi .............................. OSTADH RAMADHANI NASORO ANATUMIA  Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako, Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, DAWA za ASILI na DAWA za KIARABU, Pia ni mkuvunzi wa kutafsiri Ndoto. Pia anatoa pete za bahati zilizo amb

Harmonize "Nina Deni la Mafanikio yangu kwa Mungu na Diamond Platnumz"

Image
Huku akiwa kwenye mahojiano Harmonize alidai kwamba anamheshimu Diamond sana na kwamba ana mshukuru kwa kukuza taakuma yake ya mziki. "Licha ya kuwa kaka na rafiki yangu, kama katika uhusiano mwingine wowote hatuko karibu tena na ni jambo la kawaida. Sina lolote dhidi yake. Namheshimu sana Diamond kwa kunitia moyo na kunishauri kimuziki. Nina deni kwake kwa kuwa chanzo cha mafanikio ya muziki wangu,” alisema Harmonize. Aliongeza zaidi kuwa; "Nilipokuwa chini wakati wa hatua za awali za kazi yangu ya muziki, tulikuwa hatutengani. Diamond alijitahidi sana kuunga mkono na kukuza kazi yangu ya muziki. Nina deni la mafanikio yangu kwa Mungu na Diamond,” anasema na kuongeza kuwa kama ishara ya kumshukuru ana tattoo ya Diamond kwenye mkono wake." from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/fzQoZes via IFTTT

Nimemsomesha, Nimegharamika, Leo Kaniacha Anaolewa na Mtu Mwingine

Image
Wakuu nilikutana na huyu binti miaka kadhaa iliyopita mimi nikiwa nimepangiwa kazi mkoa fulani katika mihangaiko yangu nikakutana na huyu binti nilitokea kumpenda, mzuri kisura na kitabia very innocent niliamini kwake nimefika baada ya kash kash nilizopitia katika mahusiano ya nyuma. Wanasema usiusemee moyo ila najua yule binti alinipenda kidhati tena moyoni kabisa na mimi kwangu she was a queen na niliapa kumuoa baada ya yeye kumaliza masomo yake. Binti huyu kwao ni familia maskini nikisema familia maskini ni familia maskini kisawasawa. Baba yake alifariki miaka kadhaa nyuma kabla sijaonana nae hivyo aliishi na mama yake na wadogo zake ni story ndefu kuhusu familia yao. Mimi nikawa ndio kama msaada katika familia yao, sikua na hiyana na nilisaidia niwezavyo kwani binti yule nilimpenda kutoka moyoni. Yule binti alimaliza shule na kuhitajika kwenda chuo lakini familia ikawa haina uwezo wa kumsomesha na mkopo alikosa. Akakosa raha na ikawa kama jukumu ni langu. Mama yake aliniita tu

Rais Samia Atangaza Maombolezo ya Kitaifa Tanzania Kufuatia Kifo cha Rais Mstaafu Mwai Kibaki

Image
Taifa jirani la Tanzania linaadhimisha siku mbili za maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa taifa hilo litamuomboleza Kibaki kwa siku mbili na kuwataka Watanzania kusimama na Wakenya Kenya nayo ilitangaza Aprili 29 kuwa likizo ya kitaifa kutoa nafasi kwa Wakenya kumuomboleza rais wao wa tatu aliyefariki akiwa na umri wa miaka 90 Tanzania inaadhimisha siku mbili za maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki kilichotokea Ijumaa, Aprili 22, akiwa na umri wa miaka 90. Rais Samia Atangaza Maombolezo ya Kitaifa Tanzania Kufuatia Kifo cha Rais Mstaafu Mwai Kibaki Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku mbili za maombolezo nchini Tanzania kufuatia kifo cha Mwi Kibaki. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa tangazo hilo na kutuma risala za rambirambi kwa taifa la Kenya kwa kumpoteza kiongozi. Kupitia kwa taarifa iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ikulu ya Rais Yunus Zuhura, R

Haji Manara Atoa Mpya "Huo ukimya wa SIMBA kuelekea Mechi Yetu na wao Mnaujua Chanzo chake?"

Image
Maneno ya Haji Manara kuelekea Mechi ya Yanga na Simba: "Huo ukimya wa Makolo mnaujua chanzo chake? Hii mechi Yanga ndio Mwenyeji wa mchezo,,na kwa mujibu wa utaratibu,,Team Mwenyeji hupata mzigo wote baada ya yale makato ya kikanuni kwa Taasisi nyingine. So Kwa akili yao wanaona kukaa kimya kwao na kutosema lolote labda Washabiki wao hawatakuja, wakiamini Mapato ya Jumamosi yatapungua. Niwahakikishie Yanga tunatosha, tupo wa kumwaga,,tutaujaza Uwanja bila hata kolo mmoja kuwepo. Sisi tuna watu, na watu wenyewe ndio Wamiliki wa Nchi hiii. Mkija au mkisusa hizo sio sheeda zetu Wananchi, We Are Yanga Afrikaaaaaaaaaaaaa Au kama vp njooni na uchawi wenu wa moto watu wasije Lupaso Jumamosi" Manara from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1BGN6Aq via IFTTT

Vanessa Kuja Bongo Afunguka "Sijamzika Kaka Yangu, Sijamleta Shemeji Yenu, Sijamleta Seven"

Image
Kupitia Insta Live aliyofanya, Mwanamuziki Vanessa Mdee amemjibu shabiki aliyeuliza ni lini Msanii huyo atarudi Tanzania, Vanessa amedai atakuja nchini hivi karibuni, kuna vingi vinamfanya aje, kwanza hakuwepo wakati wa mazishi ya kaka yake,pili bado hajamleta shemeji yetu Rotimi  pamoja na Seven (mtoto wao, Vee & Rotimi). Hivyo lazima aje Tanzania hivi karibuni. Unammis kwa asilimia ngapi, Vanessa Mdee kwenye game? from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/fRwAl2v via IFTTT

Simba Yapata Balaa Jingine, Kiongozi Afrika Kusini Aishitaki CAF Kisa Moto Uwanjani

Image
Klabu ya Simba iliwasha moto uwanjani kwenye pambano lao dhidi ya Klabu ya Orlando Pirates MTENDAJI MKUU wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Afrika Kusini Tebogo Motlanthe amesema kitendo cha Klabu ya Simba kutoka Tanzania kuchoma kitu katikati ya Uwanja ni jambo la aibu na si la kiuanamichezo. Motlanthe amesema kitendo hicho hakikubaliki na tayari kama Shirikisho tayari wameandika barua kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuona hatua stahiki zinachukuliwa. Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Afrika Kusini Tebogo Motlanthe Klabu ya Simba ilitolewa na Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 katika michezo yote miwili ya hatua hiyo ya mtoano. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/PkO4nJe via IFTTT

Mwinyi Amfunda Polepole Alipokwenda Kuaga Kuelekea Malawi Kuanza Kazi

Image
RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amemueleza Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole umuhimu wa kwenda kuifanyia kazi na kuipa kipaumbele Sera ya Diplomasia ya Uchumi nchini humo. Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo alipokutana na Balozi Polepole Ikulu ambaye alikwenda kuaga tayari kuelekea katika kituo chake kipya cha kazi nchini Malawi. Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi amesema kwa sasa Tanzania imeelekeza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi na nchi za nje ambayo ndio dira ya ushirikiano na nchi nyingine kiuchumi. Amemsisitiza kiongozi huyo kwenda kuifanyia kazi sera hiyo nchini Malawi hasa katika sekta ya biashara. “Zanzibar ina mazao mengi yanayotokana na bahari ambayo ni bidhaa muhimu katika biashara nje ya nchi wakiwamo dagaa ambao bado hawajapata soko Malawi,” amesema. Amesema kwa sasa biashara ya dagaa zinazotoka Zanzibar zinafanyika zaidi katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC). Pia amemweleza kuwa

Kisa Mayele Pablo Afanya Kikao na Inonga, Amjaza Upepo

Image
MARA baada ya kikosi cha Simba kutua nchini, haraka Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mhispania, Pablo Franco alifanya kikao kizito na wachezaji wake wote kambini akiwemo Mkongomani, Hennock Inonga katika kuelekea Kariakoo Dabi. Dabi hiyo inatarajiwa kuzikutanisha timu kongwe za Simba dhidi ya Yanga, mchezo ambao utapigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo tishio kubwa hadi sasa kwa mabeki wa Simba ni uwezo mkubwa wa kutupia mabao anaouonyesha Fiston Mayele ambaye amefunga 12 kwenye ligi kuu. Kikosi cha Simba kilirejea nchini juzi Jumatatu kikitokea Afrika Kusini walipokwenda kucheza mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Simba waliondolewa na Orlando Pirates kwa penalti 4-3. Mmoja wa mabosi wa benchi la ufundi la timu hiyo, ameliambia Championi Jumatano kuwa kocha huyo katika kikao hicho kikubwa aliwataka kusahau matokeo ya mchezo uliopita dhidi ya Pirates na badala yake kuelekeza nguvu katika dabi.   Beki wa kati wa klabu ya Sim

Timu ya Man United Yaendelea Kutaabika

Image
Kuelekea mchezo wa 35 kwa Man United kunako EPL msimu huu, orodha ya majeruhi inaongezeka kwenye kikosi cha timu hiyo. United watakua uwanjani Alhamisi hii kuchuana na Chelsea ndani ya Old Trafford. Kwa hali ilivyo, The Red Devils inawakosa takribani wachezaji 6 wa kikosi cha kwanza. Kocha Ralf athibitisha. Pogba, Maguire, Sancho, Shaw, Fred na Cavani wote watakosekana kwenye mchezo huu wakati ambao, Wan Bissaka huenda akakosekana na hivyo orodha kuongezeka zaidi. Hili ni pigo kwa Rangnick ambaye anatoka kwenye vipigo vitatu kwenye michezo 4 iliyopita, anakwenda kuchuana na The Blues. Kutokana na idadi ya majeruhi kwasasa kwenye kikosi cha Man United, Ralf Rangnick amethibitisha kuwepo na wachezaji 14 tu (pamoja na chipukizi) kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Chelsea hali ambayo inampa mashaka kuelekea mwishoni mwa msimu. ✍️: @omaryramsey #SNSSports⚽⚽ from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/o7jlpD4 via IFTTT

UMEWAHI Kujiuliza Nini Lengo La Mfuko Mdogo Mbele Ya Suruali Yako Ya Jeans?

Image
Je unaujua mfuko mdogo katika suruali yako ya Jeans? Ndiyo, ule ambao umeshonwa juu kidogo ya mfuko mkubwa wa kulia. Umewahi hata mara moja kusimama na kujitafakari kwa nini huo mfuko mdogo mbele ya suruali yako ya jeans upo hapo ulipo na nini hasa lengo la mfuko huo zaidi ya pengine kudumbukiza sarafu au jojo ambayo unataka kuja kuitafuna baadae au kuwaza kama ni fasheni tu katika nguo? Kama hujawahi kujiuliza hilo swali na bado hujui chanzo na lengo la mfuko huo mdogo mbele ya suruali yako ya Jeans usijali kwani  tovuti hii itakueleza chanzo na lengo la mfuko huo. Mfuko huu ulikuwa unatekeleza jukumu muhimu sana miaka ya nyuma na ndio sababu kubwa iliyopelekea watengenezaji wa suruali za Jeans kuweka mfuko huo juu kidogo ya mfuko wa mbele wa suruali. “Ni mfuko maalum wa kuhifadhi saa. Ndiyo, inasemekana miaka ya nyuma ya 1,800, watu wengi walikuwa wanapenda kuvaa saa zao katika cheni na kuzifungia katika viuno vyao. Ili kuweza kuweka salama saa zao zisivunjike na kuharibik

Mamlaka ya Dawa "Mauzo ya Dawa za Nguvu za Kiume yapo Juu"

Image
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imesema tafiti za hivi karibuni zimethibitisha kuwa dawa za kuongeza nguvu za kiume zinaongoza kuuzwa katika maduka ya dawa nchini. Akizungumza katika kikao kazi cha Wahariri wa habari na TMDA jijini Mbeya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Adam Fimbo amesema dawa inayofuata kwa kununuliwa zaidi ni ya kuzuia kushika mimba maarufu P2. Hata hivyo, Fimbo amesema licha ya dawa hizo kuuzwa sana, watumiaji wake wanatumia kinyemela na siri kubwa bila ushauri wa daktari hali inayosababisha vifo vya ghafla. "Matumizi ya dawa hizo kwa sasa ni makubwa na sisi Mamlaka tumethibitisha kupitia tafiti kuwa mauzo yapo juu na zinatumiwa sana, tena kwa kificho hali ambayo ni hatari kwa kuwa wengi wanazidisha dozi," alisema. Katika hatua nyengine kwenye mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewahimiza TMDA kuchukua hatua za haraka, katika kudhibiti matumizi yaliyopita kiasi ya tumbaku. "Vyombo vya habari vishiriki katika kufanya uch

Wema Aibua Sababu Mastaa Kutoolewa, “Mastaa Waponzwa na Tabia zao za Kuiga”

Image
Wema Isaac Sepetu wengine wakimuita Tanzania Sweetheart au Last Born wa Taifa. Kuwa na mwenza maishani ni jambo zuri kwa kila mwanamke au mwanaume. Kupata mtu wa kukuoa au kuoa ni baraka. Inakuwa ngumu wakati watu wanazeeka, lakini hakuna wa kumpenda au kumpa hisia zake kama mwanamke au mwanaume. MASKINI WEMA Ndivyo ilivyo kwa Wema Isaac Sepetu wengine wakimuita Tanzania Sweetheart au Last Born wa Taifa ambaye ni supastaa grade A wa Bongo Movies. Maskini Wema; bidada amewashangaza mashabiki wake baada ya kutoa kilio chake cha kukosa mwanaume wa kumuoa akidaiwa kutonesha vidonda vya mastaa wengi kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo ambao hawajaolewa.   Wema anasema kuwa anatamani kuolewa, lakini tatizo pekee ni kwamba hakuna mwanaume wa kumuoa. WEMA: TATIZO BWANA HARUSI “Jamani natamani kuolewa…Yaani nimetamani tu harusi….Na iwe exquisite…the thought of me in a wedding dress, watu wamependeza…food and drinks na good music…Daaaaah… “Bibi Harusi nipo, tatizo ni bwana h

Tigo Wasaini Mkataba wa Kupanga Jengo la PSSSF Ambalo ni Refu Kuliko Yote Afrika Mashariki

Image
Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Tigo, CPA Innocent Rwetabura (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba baada ya kusainishana mkataba huo katika hafla iliyofanyika Jengo Jipya la PSSSF.  DAR ES SALAAM. Tarehe 27 Aprili, 2022. Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidijitali nchini, Tigo Tanzania, imesaini mkataba wa kupangisha Jengo la PSSSF Tower Commercial Complex ,  kati ya MIC Tanzania PLC na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa nia ya kupanua wigo na kuharakisha  utoaji wa huduma ambapo sasa watahama Jengo la Derm Complex kwenda ofisi kubwa jengo la   PSSSF Floor ya 30 hadi 33 linalopatikana Kiwanja namba 3 , Barabara ya Sam Nujoma Sinza – Dar Es Salaam Tanzania. Akizungumza kabla ya kusaini Mkataba huo CPA Innocent Rwetabura, CFO na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo amesema kuwa; “Lengo la kuhamia katika jengo hili ambalo nimearifiwa kuwa ndio jengo refu kuliko yote Afrika ya Mashariki, ni kuziweka sehemu moja timu zili

DC Sengerema Atoa Ufafanuzi Kisiwa Kinachodaiwa Kutembea

Image
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga akitoa ufafanuzi juu ya kisiwa kinachodaiwa kutembea wilayani humo Sengerema. Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga amesema hakuna kisiwa kinachotembea kijiji cha Kahunda Kata ya Katwe wilayani humo bali ni kipande cha aridhi kilichomeguka na kuingia ziwani. Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano April 27, 2022 alipokuwa akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake ili kutoa ufafanuzi juu kisiwa hicho. Ametoa ufafanuzi huo baada ya wananchi kudai kuwa kisiwa hicho kilichopo katika kijiji cha Kahunda Kata ya Katwe kinatembea. Ametoa rai kwa wananchi wanaokwenda ndani ya kipande hicho kuchukuwa tahadhari na kuwataka wataalamu wanaohusia na masuala ya aridhi pamoja na jiolojia kufika katika eneo hilo ili kitoa ufafanuzi zaidi. Senyi amesema kuwa jana alikwenda katika kijiji hicho na kamati ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kujiridhisha juu ya taarifa hizo huku akisema kuwa waligundua hakuna kisiwa kinachotembea ndani ya ziwa Victoria

"Natamani Kajala Arudi, Najisikia Vibaya" Ibraah Amuomba Kajala Msamaha Kwa Niaba ya Harmonize

Image
Mwanamuziki Ibraah wa Konde Music Worldwide ameweka bayana kuwa angependezwa sana na kufufuka kwa mahusiano kati ya bosi wake Harmonize na mwigizaji Fridah Kajala Masanja. Ibraah ambaye kwa jina halisi ni Ibrahim Abdallah Nampunga amekiri kuwa moyo wake unaumia kuona jinsi mdosi wake anavyohangaika. "Kwa kweli natamani Kajala arudi nyumbani kwa sababu ni furaha ya ndugu," Ibraah alisema akiwa kwenye mahojiano na Carrymastory. Ibraah aliweka wazi kuwa kwa kawaidai huwa hahusiki na masuala ya kifamilia ya Harmonize na hana ufahamu mzuri wa yaliyotokea kati yake na Kajala. Hata hivyo alimwomba mwigizaji huyo msamaha kwa niaba ya bosi wake na kumsihi amrudie. "Kama binadamu, kwa kweli najisikia vibaya kwa sababu ndugu anajisikia vibaya. Kama ingewezekana kumwomba msamaha basi namimi nimwombe msamaha Kajala. Msamehe kakangu kama alikukosea," Alisema. Mwanamuziki huyo alipuuzilia mbali madai kuwa Harmonize ametia bidii kubwa zaidi katika kurejesha mahusiano

Pablo: Simba Tulieni, Tunawapiga Yanga Jumamosi Uwanja wa Mkapa

Image
WAKATI Simba SC wakitua Dar wakitokea Afrika Kusini, kocha mkuu wa kikosi hicho, Pablo Franco, akilini mwake alikuwa akiiwaza Yanga kuelekea mchezo wa Jumamosi hii, huku akiwaambia mashabiki wa Simba watulie, ushindi upo.   Pablo ambaye hii itakuwa ni mara ya pili kukutana na Yanga tangu atue Simba baada ya awali kutoka 0-0, ameweka wazi kuwa, wanaelekeza nguvu zao katika mchezo huo kwa lengo la kupunguza pengo la pointi na wapinzani wao hao, hivyo lazima washinde.   Pablo ametoa kauli hiyo kufuatia Simba juzi Jumapili kuondolewa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.   Simba inatarajia kucheza na Yanga Aprili 30, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar. Yanga wanaongoza ligi kwa pointi 54, wakati Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 41. Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo alisema nguvu na mapambano kwa sasa wanaelekeza katika mechi zao za li

Shaffih Dauda "Simba wanaweza kuiangalia TP Mazembe kama timu ya mfano kwao"

Image
Kushinda ubingwa wa Afrika au kuwa na matokeo mazuri mfululizo kwenye mashindano ya CAF Champions League au Confederation Cup ni jambo linalohitaji muda. Simba wanaweza kuiangalia TP Mazembe kama timu ya mfano kwao, vilevile naamini hata Mo role model wake ni Moise Katumbi kwa namna ambavyo aliichukua Mazembe na kuifikisha hatua ya kushinda mataji ya Afrika. Katumbi aliichukua TP Mazembe mwaka 1997 lakini mwaka 1998, 1999 na 2000 Mazembe haikushiriki kabisa mashindano ya CAF. Mwaka 2001 Mazembe ilishiriki CAF Champions League kwa mara ya kwanza tangu Katumbi amekuwa Rais wa klabu! Wakifika hadi Makundi na kushika mkia kwenye Kundi A. Mwaka 2002 Mazembe ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi ndio mafanikio ya kwanza baada ya uwekezaji wa miaka mitano. Mwaka 2004 wakatolewa mapema na Zamalek, 2005 wakatolewa tena hatua ya awali, 2006 hawakushiriki kabisa! Mwaka 2007 waliishia raundi ya pili wakatolewa na Rabat. Mwaka 2008 wakafika hadi hatua ya makundi na kumaliza katika nafasi y

Msanii Wizkid Akunja Zaidi ya Shilingi Bilioni 2 Kuwa Msanii Kinara Tamasha la Rolling Loud

Image
Mwimbaji wa Nigeria Wizkid ametajwa kwenye orodha ya wasanii watatu vinara (headliners) ambao watatumbuiza kwenye tamasha la Rolling Loud ambalo litafanyika September 9-11 mwaka huu mjini Toronto Canada. Mbali na Wizkid kuna Future na Dave ambao ndio wanakamilisha idadi ya headliners watatu wa tamasha hilo lenye mamia ya wasanii wakali toka nchini Marekani ambao watapanda Jukwaani. Kubwa hapa ni kiasi cha pesa ambacho Wizkid amelipwa kutumbuiza kama msanii kinara, kupitia insta story yake amesema amelipwa ($1 million) zaidi ya Shilingi Bilioni 2.3 za Kitanzania. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/y3YREUN via IFTTT

Simanzi; Miili Ya Wanakwaya Waliokufa Ajalini Njombe Yaagwa

Image
SIMANZI na majonzi! Miili tisa ya waumini wa Kanisa Katoliki mkoani Njombe waliofariki kwa ajali ya gari iliyotokea Kijiji cha Igima wilayani Wanging’ombe Aprili 24, 2022 imeagwa katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Njombe. Akizungumza wakati wa ibada ya kuaga miili hiyo leo Jumanne Aprili 26, 2022, Mkuu wa Mawasiliano wa Jimbo hilo, Padri Eusebius Kyando amesema Umoja wa Vijana Katoliki Jimbo la Njombe (Uvikanjo) pamoja na walezi wao walipata ajali wakiwa wanarudi katika safari yao ya kitume walikokwenda kuwatembelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Dorothea Upendo kilichopo Ibumila Parokia ya Mtwango. Amesema katika ajali hiyo, watu watatu walifariki papo hapo na wengine sita walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu hospitalini. Amesema toka mwaka 2020 Uvikanjo Parokia ya Njombe wamekuwa wakifanya kazi ya utume kwa kutembelea jumuiya ndogondogo na watu wenye mazingira magumu na kufanya matendo ya huruma katika vituo hivyo. “Vijana wetu walipa

Enyi Wadada wa Mjini Maisha yamebadilika Mwenye Masikio na Asikie

Image
Maisha yamebadilika, nyakati zimebadilika ela za mchezo hazipo tena kila senti inakazi ya kufanya. Enyi wadada mliozoea mizinga jifungeni Mikanda mwafwaaa. Ile ya baby naomba unitumie elfu 30 kwenye MPESA hizo zama zimepita, hyo ela ukiihitaji itabidi uje uifanyie kazi haswa, itabidi ufue, Utandike kitanda, upike na game uperform Vizuri. Maisha ya ujanja ujanja yamepita nasema na mwenye masikio asikie from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/301JmtU via IFTTT

Wanaume Waongoza Vifo Vitokanavyo na Ukimwi

Image
Dar es Salaam. Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (ATF) umesema vifo vitokanavyo na Ukimwi vimekua vikiongezeka miongoni mwa wanaume wenye maambukizi, huku tabia hatarishi zikitajwa chanzo. Hata hivyo, vifo hivyo vimetajwa kuendelea kupungua miongoni mwa wanawake waliopata maambukizi hayo. Hayo yamesemwa leo Aprili 25, 2022 na Meneja wa Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (ATF) Peter Kivugo alipokuwa akitoa mafunzo kwa waandishi na maofisa masoko wa vyombo vya habari juu ya dhana ya serikali ya uanzishwaji wa mfuko huo. “Vifo vinavyotokana na magonjwa nyemelezi kwa wanawake vimepungua lakini kwa wanaume vinapanda, wengi wanakufa mapema kutokana na kushindwa kuzingatia maelekezo ya dawa na kujizuia katika tabia hatarishi ambazo zinawasababisha kupata maambukizi mapya na magonjwa mengine ya zinaa,” amesema Kivugo. Kivugo ametaja takwimu za vifo vitokanavyo na Ukimwi kwa mwaka 2019 watu wazima miaka 15 na zaidi vilikuwa 21,529 ambapo wanaume walikuwa 12,225 n

Kutana na Miujiza ya Mtaalam Bahati Kutoka Morogoro, Mtaalam wa Tiba Asili Tanzania na Duniani Kote

Image
KUTANA NA MIUJIZA YA MTAALAM BAHATI KUTOKA MOROGORO MTAALAM WA TIBA ASILI TANZANIA NA DUNIANI KOTE (Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU MTAALAM BAHATI KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI: MTAALAM BAHATI ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, 🔥anatumia kitabu cha quran dawa za asili dawa za kiarabu, na majini, 🔥Anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, anazo dawa za mapenzi, 🔥nguvu za kiume, chango kwa kina mama, ngiri maji na n.k, 🔥anakuvutia mali zilizo potea au kudhulumiwa, pia anatoa pete za bahati, zilizoambatanishwa na jini mali, Wenye matatizo ya uzazi, jini mahaba, mapepo ya kichawi, vifungo vya kimaisha, ndoto mbaya za usiku, uelewa mdogo wa ufahamu shuleni kwa watoto wote, 🔥pia anauwezo mkubwa wa kumaliza kazi zilizoachwa na wataalamu wengine ndani ya masaa 48 tu, Pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo. WASILIANA NAE KWA SIMU NO: +255 719 626 586 WhatsApp no: +255 719 626 586 USH

Star Wa Filamu Nchini Tanzania Irene Uwoya Kufunga Ndoa Ingine

Image
Star Wa Filamu Nchini Tanzania Irene Uwoya Ameonesha Hamu ya Kufunga Ndoa Kwa Mara Nyingine Tena Kupitia Ukurasa wake Wa Instagram Ameandika haya Hapa: "I can't wait for My Wedding, I Love You @krishndiku08" - Uwoya Hii inaonyesha Kuwa Kuna Kitu kinakuja huenda Amepata mchumba Mpya , wazungu Wanasema time will tell Hii Itakuwa Ni Ndoa Ya Pili Baada Ya Kuvunjika Ile Aliyofunga Mwanamuziki Dogo Janja Ambayo ilidumu Kwa Muda mchache Sana from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/SCR2GrN via IFTTT

Hatimaye Channel ya Youtube ya Msanii Diamond Platnumz imerejea Tena Hewani

Image
Hatimaye channel ya youtube ya msanii @diamondplatnumz imerejea tena hewani katika mtandao wa youtube baada saa kadhaa kuondolewa na youtube wenyewe. Channel hiyo ambayo ina siku mbili tangu idukuliwe (hacked), mapema leo ilikuwa imeondolewa na youtube (terminated) kufuatia kukiuka masharti na kuvunja sheria zilizowekwa na youtube. Mkuu wa Kitengo cha Digital katika kampuni ya WCB, @kimkayndo mapema leo alifunguka sababu za youtube kuiondoa channel hiyo, ambapo alisema; "Kutokana na live iliyoruka siku ya Jumapili pindi channel hiyo ilipokuwa imehakiwa na kutoa maudhui yaliyovunja sheria za Youtube" alieleza @kimkayndo kupitia ukurasa wake wa twitter. ✍️: @omaryramsey from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/O05RPzT via IFTTT

Rapa Megan Thee Stallion Alinipiga Risasi Kisha Akaniambia Nisiseme Atanipa Bilioni 2"

Image
Rapa Megan Thee Stallion ameendelea kufunguka ambayo hatuyafahamu kwenye shtaka lake la kupigwa risasi ya mguu na Tory Lanez Julai 12 mwaka 2020 Jijini Los Angeles, shtaka ambalo bado linaendelea mahakamani. Leo (April 25) Televisheni ya CBS imeachia mahojiano yote ya Megan Thee Stallion ambayo alifanya na Gayle King, alisema Tory Lanez alijaribu kumfumba mdomo kwa kutaka kumpa kiasi cha ($1M) zaidi ya TSh. Bilioni 2.3 ili asiwaambie polisi kuwa ndiye aliyempiga risasi. “Aliomba radhi, alisema samahani sana tafadhali usimwambie mtu yeyote, nitakupatia ‘Dola Milioni’ kama hutosema chochote.” alieleza Megan Thee Stallion kwa uchungu huku akifuta machozi. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Mrf2FGY via IFTTT

Rais Samia asema anazielewa sababu Chadema kususia

Image
Rais Samia Suluhu Hassan RAIS Samia Suluhu Hassan amesema anaelewa sababu ya chama kimoja ambacho hajakitaja, kimekataa kushiriki mchakato wa majadiliano ya kutafuata muafaka mazingira ya ufanyaji siasa na kuleta umoja wa kitaifa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Rais Samia ameyasema hayo jioni ya Jumamosi tarehe 23 Aprili, 2022 wakati akizungumza na Watanzania waishio Marekani (Diaspora), Washington DC na kueleza kuwa bado anaendelea na majadiliano nao ili wajiunge na wenzao. “Tumeanza mazungumzo na vyama vya siasa kupitia baraza lao la siasa tumefamnya mkutano wa awali na kuunda kikosi kazi chao wenyewe watajadili mambo ambayo wenyewe wamepanga watatuletea. “Kuna chama cha siasa kimoja bado hakijakubali, bado naendelea na mazungumzo nao na naelewa kwanini hawajakubali moja kwa moja kujiunga bado naendelea na mazungumzo nao tunakwenda vizuri na namatumaini watajiunga na wenzao,” amesema Rais Samia.   Rais Samia ambaye alipokewa na mabango na baadhi ya Watanz

Well Done Inonga...Simba Wanahitaji Roho na Damu Kama Hizi Tano Kwenye Timu

Image
Unahitaji roho na damu kama hizi tano kwenye timu, unahitaji chui kama hawa watano kwenye timu yako Mmoja anatuliza mstari wa ulinzi, wawili wanatuliza mstari wa kati, mmoja mwishoni anamwambia Sakho asipake sana rangi upepo Kisha mmoja kwenye bench anaingia kama game changer Yes wanae mmoja tayari wamalizie na wanne kwenye dirisha la usajili, unahitaji wakatili wengi kama INONGA Shaffih Dauda from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1MFZ2i3 via IFTTT

Mbinu Tuliyotumia Tukabadilisha Maisha Yetu. Hukuna kujuta tena

Image
Wananiita Priscilla Kisham na bwanangu ni mfanyabiashara mashuhuri ambaye ana magari za abiria nyingi mno na kwa siku yeye hutengeza hela nyingi anazoziweka kwa hazina ya benki.  Kwa kweli sisi ni matajiri! Lakini kumbuka kuwa tulipopatana naye huko Bukoba alikuwa mtu maskini asiyejiweza; hata chakula cha kila siku ikawa ni ndoto kwetu kwani mara nyingi  tungelilala njaa kana kwamba hatuna kisomo chochote. Mimi nimesomea taaluma ya Marketing naye amesomea uahandisi lakini kupata kazi  ikakuwa ni vigumu jambo lililofanya aanze kufanya biashara rejareja mtaani kwetu. Aling’ang’ana mno kwa miaka tatu bila mafanikio na hadi tukaanza kufikiria kurudi nyumanii mashambani. Hali ilibadilika ikawa hata ngumu zaidi wakati kulipa kodi ya nyumba ilikuwa vigumu na mwenyewe hata akaiweka kufuli.  Tulilala kwa jirani siku hiyo na siku iliyofuata asubuhi tukafunganya virago kurudi kwetu mashamabani. Ilikuwa aibu kubwa! Maisha magumu ilituzonga na kutuandama hadi huko mashaambani

Mapya Yafichuka Rubi iliyo Mnadani Dubai

Image
SERIKALI imetoa ufafanuzi juu ya jiwe la rubi linalosemekana kusafirishwa kwenda Dubai kutoka Tanzania kwa ajili ya kupigwa mnada na inafanya uchunguzi kujua mmliki halisi wa jiwe hilo na nchi lilipotoka. Hayo yalielezwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko alipokuwa akizungumza jijini Dodoma katika semina ya madini kwa wabunge wanawake. Biteko aliwataka Watanzania wawe watulivu wakati serikali inaendelea kufanya uchunguzi kujua kama kweli jiwe hilo pamoja na mengine 25 yaliyogundulika baadaye yanatoka Tanzania kwa kuwa serikali haiwezi kutoa majibu ya haraka bila kujua lengo la taarifa hiyo iliyotangazwa kupitia kituo cha televisheni cha News24 Akifafanua jambo hilo. Biteko alisema baada ya kuona taarifa hiyo kwenye mitandao walichukua hatua ya kuhakiki katika mfumo wa usafirishaji madini lakini hakukuwa na taarifa ya kusafirishwa jiwe hilo kwenda Dubai hivyo wakaamua kuwasiliana na kampuni ya SGA Dubai inayohusika na jiwe hilo wakawaeleza kuwa jiwe hilo walilipata kutoka Marekan

Huyu Ndio Snitch Aliyemchoma ASAP Rock Mchumba wa Rihanna Mpaka Kukamatwa na Polisi

Image
Member wa kundi la ASAP [ Always Strive And Prosper] ASAP Bari amesema anauhakika shahidi aliyetoa maelezo kwa polisi yaliyopelekea A$AP Rocky kukamatwa na kuhojiwa ni mmoja wa watu kutoka kwenye kundi lao la ASAP Mob anaefahamika kama ASAP Relli. Haijulikani alichosema ASAP Relli kwa polisi ila ushahidi wake ulipelekea A$AP Rocky kukamatwa. ASAP Relli ni member wa ASAP Mob, ni mmiliki wa lebo ya muziki na burudani ya Shuteye Entertainment. Toka taarifa za yeye Ku-Snitch kusambaa ameweka IG Yake Private na kukaa mbali na wasanii wengine wa hiphop. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/gxLlbhi via IFTTT

Diva na Mumewe Wapata Ajali Mbaya ya Gari "Tunaendelea na Matibabu"

Image
From Divatheebawse: Asante kwa raia waliotusaidia with alot of love maana i was devastated .. and thanks @iamnellyg5 Ni Mungu tu!. leo tunaendelea na matibabu .... maisha ya Mwanadamu ni mafupi sana nimeona jana. bajaj au Pikipiki wakiendelea achiwa wataendelea sababisha vifo vya wengi sana ... Siwez ata kulala naona ile bajaj ikipanda juu ya kioo cha gari and the blood ... it was scary Mungu wangu🥲 ila Mungu anatupenda sana Kwa Ule mzinga tumetoka wazima Ni kudra zake mwenyezi Mungu na msaada tumepata kwa mapenzi sana makubwa ya watu .. nimepost kushukuru watu raia wa kawaida kabisa ambae walitu take care na kuhakikisha kila kitu chetu kiko salama na sisi tuko salama hatuna cha kuwalipa kabisa zaid ya shukran za upendo kwenu!. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/vNBl7SX via IFTTT

Wema Sepetu "Jamani Natamani Kuolewa... Yaani nimetamani tu Harusi"

Image
Jamani Natamani Kuolewa... Yaani nimetamani tu Harusi.... Na iwe Exquisite... The thought of me in a Wedding Dress, watu wamependeza... Food & Drinks na Good Music... Daaaaah... Trust me natamani Sana na Watu Wengi watanichangia Siwezi Kufanya harusi Bila kuchangisha watu mie Mwenyewe nimechangia Watu Wengi sana Bibi Harusi nipo, Tatizo ni Bwana Harusi.... Bado hajajitokeza... from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/LbTaXZH via IFTTT

Madiwani 41 Moshi Wamkataa Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo

Image
Moshi. Madiwani 41 wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameandika barua ya kumkataa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kastory Msigala wakimtuhumu kufanya maamuzi binafsi kupitisha baadhi ya miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo. Madiwani hao walioandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha barua yao, wanalalamikia ukusanyaji wa mapato hafifu kutokana na utendaji usio shirikishi wa mkurugenzi huyo pamoja na utolewaji wa maamuzi ya utekelezaji wa miradi bila kushirikisha kamati ya fedha na baraza la madiwani. Hatua hiyo imefikiwa ikiwa zimepita siku chache tangu madiwani wa Manispaa ya Moshi mkoani hapa, kupiga kura za kumkataa Meya wa Manispaa hiyo, Juma Raibu. Akizungumza jana baada ya kikao cha madiwani kilichokaa ofisi za CCM wilayani Moshi, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Moris Makoi alisema tatizo hilo ni la muda mrefu na wamekuwa wakimlalamikia lakini hakuna mabadiliko, ndiyo maana wameamua kuandika barua hiyo. “Fedha za halmashauri zinapoletwa ku

Rais mstaafu Honduras Apelekwa Marekani Kwa Tuhuma za Madawa ya Kulevya

Image
  Rais wa zamani wa Honduras amepelekwa Marekani ili kukabiliwa na madai ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, chini ya miezi mitatu tu baada ya muhula wake kukamilika.  Juan Orlando Hernandez amekabidhiwa kwa maafisa wa Marekani wa kitengo cha kukabiliana na mihadarati katika uwanja wa ndege ulioko katika mji mkuu Tegucigalpa.  Hernandez mwenye umri wa miaka 53 mbali na madai ya ulanguzi wa mihadarati atakabaliwa na mashtaka ya kusafirisha silaha Marekani kinyume cha sheria.  Anadaiwa kusaidia katika ulanguzi wa kilo laki tano za madawa ya kulevya ya cocaine kutoka Honduras hadi Marekani.  Hernandez anakanusha mashtaka hayo. Anasema walanguzi wa madawa ya kulevya wanaotaka kupokea kifungo cha muda mfupi Marekani ndio waliompangia njama hiyo. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/IXKiArY via IFTTT

Adaiwa Kumpa Dawa Mwanamke, Kumbaka

Image
MKAZI wa jijini Dar es Salaam, Borgias Kwitega, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kumwekea dawa za kupumbaza mwanamke, kumbaka na kuiba simu. Kwitega na mshtakiwa Abdallah Mmanyi ambaye anakabiliwa na shtaka la kupokea mali ya wizi, wamefikishwa jana mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemarila na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Lucy Uisso. Mshtakiwa wa pili Ally Kibuga, hakufikishwa mahakamani hapo, kwa kile kilichoelezwa kuwa bado yupo mikononi mwa polisi. Wakili Uisso alidai washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 64/2022 na katika shtaka la kwanza, Kwitega anadaiwa kumwekea vidonge vya kupumbaza mwanamke. Inadaiwa tukio hilo alitenda Januari 24, 2022 eneo la Rumix Hotel iliyopo Kinondoni, alimpa vidonge vya kupumbaza, mwanamke mwenye umri wa miaka 30. Shtaka la pili, siku na eneo hilo, Kwitega alimbaka mwanamke huyo, bila ridhaa yake. Shtaka la tatu, Kwitega anadaiwa kuiba simu aina

Hatufanyi biashara ya binadamu - Rais Kagame

Image
  Rais wa Rwanda  Paul Kagame amesema kuwa nchi yake haifanyi biashara ya binadamu, ikiwa ni maoni yake ya kwanza toka nchi hiyo iingie makubaliano ya kupokea wahamiaji kutoka nchini Rwanda Kwenye makubanliano yaliyoipo ni kwamba wahamiaji wanaosaka makazi ambao watawasili nchini Uingereza wakiwa kwenye boti ndogo, watapelekwa moja kwa moja nchini Rwanda.   Mpango huo ambao Rwanda imepokea kiasi cha Paund milioni 120  sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania  bilioni 347,umekua ukikosolewa ndani na nje ya nchi hizo.    Rais Kagame ambaye alikua na ziara katika nchi za Congo-Brazzaville, Jamaica, na Barbados wakati mpango huo ukitiwa saini amesema kuwa ni kosa kudhani kwamba Rwanda inanufaika na fedha kutokana na kupokea watu wanaosaka makazi.   “hatuuzi binadamu  tafadhali, tuanawasadiia ” amesema Rais Kagame wakati wa semina chuo kikuu cha Brown nchini Marekani . Rais Kagame amesema kwamba  Uingereza iliihitaji Rwanda kwa kwenye zoezi hili sababu nchi hiyo ina uzoefu wa kupok