Mhadhiri SAUT adaiwa kuuawa kwa kunyongwa
Mwanza. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Mwanza, Hamida Mussa maarufu 'Mama Mwakitosi' (64) anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na mtandio shingoni na mfanyakazi wa ndani ambaye alitokomea kusikojulikana baada ya tukio hilo. Mwili wa Hamida ulikutwa jana Jumanne Novemba 29, 2022 nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki wilayani Ilemela mkoani Mwanza ukiwa umelala sakafuni kifudifudi ukiwa na mtandio shingoni mwake. Taarifa zinaeleza mhadhiri huyo wa Idara ya Uhandisi Kitivo cha ICT, SAUT alikuwa anaishi na msaidizi wa kazi ambaye baada ya tukio hilo kutokea ametokomea kusikojulikana. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Novemba 30, 2022, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buzuruga Mashariki, Martin Muya amethibitisha kutokea tukio hilo. Amesema pamoja na kujua Hamida alikuwa anaishi na mfanyakazi wa ndani ila hakuwahi kumtambua kwa sura japo anajua alikuwa na umri kati ya miaka 15 hadi 18 kwani hakuwahi kumtambulisha ofisini kwake. Mtoto wa...