Hitilafu za Umeme Katika Uwanja wa Benjamin Mkapa..Hii ni Mara ya Pili
Hitilafu za umeme katika Uwanja wa Benjamin Mkapa zimeendelea ambapo leo tena zimesimamisha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Rivers United. Mchezo huo ulisimama dakika ya 25 kipindi cha kwanza zikianza kuzimika Moja kwenda nyingine kisha kumalizika zote zinazozunguka uwanja huo. Baada ya kuzimika kwa taa hizo mwamuzi wa mchezo huo Jiyed Redouane kutoka Morocco alisimamisha mchezo na timu kubaki uwanjani zikisubiri kuwaka tena kwa taa hizo. Hata hivyo baada ya dakika 6 baadaye zilianza kuwaka taratibu Moja na kuondoa giza kubwa lililokuwa uwanjani. Jiyed ilipotimu dakika 40 ambapo ni dakika 15 baadaye tangu zilipozimika alizirudisha timu vyumbani huku taa hizo zikiendelea kuongezeka kuwaka. Dakika nane baadaye mwamuzi huyo alirudi uwanjani huku taa zikiendelea kuwaka ambapo pia dakika Moja baadaye wenyeji Yanga pia walirejea na kuanza kupasha misuli na kufuatiwa na Rivers. Hii ni mara ya pili kwa taa hizo kuzimika wakati mchezo unaendelea...