Mama wa Beyonce, Tina Knowles, amefungua kesi ya kudai talaka dhidi ya mume wake wa pili, Richard Lawson, baada ya miaka nane ya ndoa yao. Tina, mwenye umri wa miaka 69, amefungua kesi hiyo Jumatano, Julai 26, akidai "tofauti zisizoweza kusuluhishwa" kama sababu ya kutengana. Tina, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Celestine Ann Beyonce, alibadilisha jina lake kuwa Celestine Lawson alipoolewa na Richard, na anataka kurudisha jina lake hilo [Celestine Knowles], jina la aliyekuwa mume wake wa kwanza. Tina na Richard walifunga ndoa Aprili 2015 na hawana watoto pamoja. Mama Bey ana watoto wawili na mume wake wa kwanza, Mathew Knowles, mwenye umri wa miaka 71, ambao ni Beyonce, mwenye umri wa miaka 41 na mwimbaji na mwigizaji Solange, mwenye umri wa miaka 37. Mwaka 2019, alitengana na baba wa watoto wake hao baada ya kudumu pamoja kwenye ndoa kwa miaka 31 kuanzia 1980 hadi 2011. Walitengana baada ya kubainika kuwa Mathew, ambaye alikuwa meneja wa binti yake Beyonce had...